dc.description.abstract | Tasnifu hii imeangazia ulinganishi na ulinganuzi wa tasfida za muktadha wa matibabu katika Kiswahili na Kimarachi. Tumejikita katika tasfida za tiba, ushauri nasaha, uhamasishaji na uasaji. Tulichagua mada hii kwa sababu ulimwengu hivi leo unakumbwa na janga la ukumwi na magonjwa mengine hatari ambayo huhitaji kuzungumziwa kwa lugha ya upole ili ujumbe uwafikie walengwa kwa njia isiyotisha, kukera au kuzua aibu. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kubainisha tasfida za muktadha wa matibabu katika Kiswahili na Kimarachi, kuangalia mfanano au tofauti za tasfida hizo na mikakati inayotumiwa kuibua tasfida za muktadha wa matibabu katika jamii lugha husika. Data kuhusu tasfida za matibabu katika Kiswahili tumeipata kwa kusoma kamusi za semi, kamusi sanifu ya TUKI na vitabu vingine vya Kiswahili sanifu tulivyopata. Data kuhusu lugha ya Kimarachi nayo tumeipata nyanjani kwa kuwasilisha hojaji kwa baadhi ya watumiaji wa Kimarachi tuliowachagua kwa njia ya kimaksudi ili wajaze. Mtafiti pia ametumia ujuzi wake kama mwanafunzi wa Kiswahili na mzungumzaji wa Kimarachi kutathmini tasfida husika. Tuliwahusisha wauguzi, watoa ushauri nasaha, wahamasishaji, waasaji na wanajamii wengine kujaza hojaji hizo. Pia, tulifanya mahojiano na wazee wachache wanaozungumza Kimarachi ambao hawajaathirika kwa vyovyote na elimu au hata kusafiri ng’ambo. Tumebainisha tasfida zinazotumiwa katika tiba na ushauri nasaha na zile zitumiwazo katika uhamasishaji na uasaji katika Kiswahili na Kimarachi kisha tukazipanga kwenye majedwali. Tumechunguza idadi ya tasfida hizi, mfanano au tofauti zake katika lugha tafitiwa na mikakati inayotumiwa kuibulia tasfida hizo. Tumechanganua data tuliyoipata kwa kutumia nadharia mbili: nadharia ya ethnografia ya mawasiliano ya Dell Hymes (1974) na nadharia ya upole ya Brown na Levinson (19 | en_US |