Show simple item record

dc.contributor.authorKimetto, Hillary K
dc.date.accessioned2017-01-05T09:17:49Z
dc.date.available2017-01-05T09:17:49Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/99143
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza ulinganifu wa taarifa za habari zinazotafsiriwa kutoka Kiswahili hadi Kikipsigis, mojawapo ya lahaja za Kikalenjin, katika kituo cha redio cha Kitwek ambacho ni kitengo cha Shirika la Utangazaji la Kitaifa (KBC). Utafiti huu ulichochewa na udadisi tuliofanya katika shirika hili ambao ulibainisha kwamba habari zinazosomwa katika kituo cha Kitwek ni tafsiri za zile zinazosomwa katika idhaa ya Kiswahili ya KBC. Utambuzi huu ulitupa mshawasha wa kuchunguza ulinganifu wa taarifa hizo. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza aina za tafsiri, matatizo yanayokumba tafsiri, vyanzo vya matatizo yenyewe pamoja na kupendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazokumba tafsiri za taarifa za habari katika kituo kilichoteuliwa. Nadharia ya ulinganifu amilifu ya Nida ilitoa msingi wa kinadharia katika utafiti huu. Aidha, nadharia ya mawasiliano ya Newmark ilihusishwa kama nadharia changizi kutokana na uhusiano uliopo kati ya mihimili yake na ile ya nadharia ya ulinganifu amilifu. Data msingi katika utafiti huu ilikuwa miswada ya taarifa za habari katika Kiswahili na katika Kikipsigis. Uchanganuzi linganishi wa miswada hiyo ulifanywa ili kutathmini ulinganifu wa maana kwenye matini za miswada hiyo. Kutokana na uchanganuzi huo, imedhihirika kwamba tafsiri maana na tafsiri mawasiliano huchangia pakubwa katika kuibushwa kwa viwango vya juu vya ulinganifu wa maana kati ya matini za lugha chanzi na za lugha lengwa ilhali tafsiri ya moja kwa moja na tafsiri huru husababisha upotoshaji mkubwa wa maana ya matini chanzi katika matini lengwa. Vilevile imebainika kwamba tafsiri za taarifa za habari ni shughuli ambayo hukumbwa na matatizo anuwai kama tofauti za kiisimu na za kitamaduni kati ya lugha chanzi na lugha lengwa, upenyezaji na udondoshaji wa vipengele vya matini chanzi katika lugha lengwa na uchangamano katika tafsiri za misemo na nahau. Pia uchunguzi wetu umedhihirisha kwamba ipo mikakati mbalimbali inayoweza kutumiwa na mtafsiri kukabiliana na changamoto hizo kama ufutaji wa dhana inayotatiza, ufafanuzi na maelezo, matumizi ya neno fidia katika lugha lengwa, matumizi ya neno la mkopo, matumizi ya dhana yenye maana ya kijumla, uundaji wa istilahi mpya, urejeleaji wa makamusi na mtafsiri kuwa na stadi za kukabiliana na changamoto za tafsiri. Utafiti huu ni mchango katika kuelewa jinsi tafsiri zinazohusisha lugha zinazotofautiana kimuundo zilivyo changamano. Utafiti huu unapendekeza kutumiwa kwa matokeo yake kama mwongozo wa kukabiliana na changamoto za tafsiri hata katika nyanja nyinginezo kwa kutilia maanani hali kwamba japo nyanja zinatofautiana kwa namna moja au nyingine, mikakati ya tafsiri katika nyanja zenyewe huingiliana.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUlinganifu Wa Taarifa Za Habarien_US
dc.titleUlinganifu Wa Taarifa Za Habari: Tathmini Ya Tafsiri Kutoka Kiswahili Hadi Kikipsigis Katika Kituo Cha Kitweken_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States