Show simple item record

dc.contributor.authorOchichi, Alice K
dc.date.accessioned2013-11-26T14:29:23Z
dc.date.available2013-11-26T14:29:23Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.citationMahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60540
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya shahada ya uzamili katika kiswahilien
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza jinsi wazungumzaji hutumia misimbo inayozua uwazi na umaanisho katika lugha za Kiswahili na Ekegusii kwa lengo la kubainisha kama kuna mlingano wowote kati ya lugha hizi, zote zikiwa lugha za Kibantu. Lugha hizo zimeelezwa kisemantiki ambapo maana msingi za kauli zimechanganuliwa, na baadaye maana za kipragmatiki kuelezwa kwa kutumia Nadharia ya Uhusiano. Nadharia ya Uhusiano ya Sperber na Wilson (1986) ilitumiwa kufasiri misimbo iliyotokana na kategoria mbalimbali za lugha hizi mbili ambapo kanuni za uhusiano pamoja na kanuni ya ujuzi wa msikilizaji zilisaidia kupata fasiri iliyokusudiwa na wasemaji wa kauli mbalimbali. Tasnifu hii ina sura nne. Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia utangulizi kwa jumla. Tumeeleza kuhusu lugha za Kiswahili na Ekegusii, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchangua mada, upeo na mipaka misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu pamoja na mbinu za utafiti tulizotumia. Katika sura ya pili, tumejadili kuhusu kategoria za kisemantiki kwa jumla ambapo tumebainisha makundi mawili makuu ya kisemantiki ambayo ni pamoja na kategoria za kileksika na kategoria za kimuktadha. Sura ya tatu imejadili kategoria mbalimbali za kisemanti ambazo huibuka kimazungumzo katika lugha ya Kiswahili na vilevile lugha ya Ekegusii na kueleza uwazi na umaanisho wa kauli hizo. Ufafanuzi wa maana kiumaanisho umefanywa kwa kutumia mbinu za kinadharia za uhusiano. Nadharia ya Uhusiano ilitumiwa ambapo ilibainika kwamba lugha hizi mbili zinatumia mitindo tofauti kuzua umaanisho. Aidha, tofauti za kiuteuzi wa maneno zimebainishwa katika lugha zote. Sababu za tofauti hizo zimejadiliwa. Katika sura ya nne, mahitimisho na mapendekezo yametolewa ambazo nadharia tete pamoja na madhumuni ya utafiti yametathminiwa. Kutokana na tathmini hizo pamoja na uchanganizi wa data yetu, tumerejelea nadharia tete zetu ambapo baadhi zimekubaliwa na nyingine kukanushwa. Vilevile, katika sura hii tumetoa mapendekezo ya tafiti za baadaye. Uchanganuzi wa misimbo mbalimbali ulidhihirisha tofauti za uteuzi wa kategoria za kisemantiki zinazotumika katika lugha za Kiswahili na Ekegusii, na maana zilizosimbwa pia zilibainisha tofauti kadha wa kadha. Hali hii ilibainishwa na tofauti za fahamu za awali za tamaduni katika lugha hizo mbili, mitazamo pamoja na mazingira ya watumizi wa lugha hizi.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUwazi na umaanisho: usimbaji maana kimazungumzo Katika ekegusii na kiswahilien
dc.typeThesisen
local.publisherIdara ya isimu na lughaen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record