• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Sababu na athari za ubadilishaji-msimbo Shuleni: Utafiti katika shule ya upili ya Akiba

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (1.199Mb)
    Date
    2010
    Author
    Wanjugu, Veronicah W
    Type
    Thesis
    Language
    en_US
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza na kubainisha sababu na athari za ubadilishajimsimbo wa lugha za Kiswahili na Kiingereza wa data iliyokusanywa kwa kurekodiwa katika Shule ya Upili ya Akiba, Kangemi, kwa kutumia nadharia ya ukubalifu wa mawasiliano ya Howard Giles. Kutokana na nadharia tete zilizoongoza utafiti huu, mambo yafuatayo yalikadiriwa: kwanza, kuwa sababu zinazochangia ubadilishaji-msimbo shuleni Akiba zinatokana na hali ya kiutambuzi; pili, kuwa sababu za kiutambuzi za ubadilishaji-msimbo zinahusiana na zile za kijamii na kibinafsi na tatu ni kuwa kuna athari zinazotokana na ubadilishaji-msimbo wenyewe. Ilithibitika kuwa, sababu za kiutambuzi za ubadilishaji-msimbo zinahusiana na zile za kijamii na kibinafsi, na pia kwamba kuna athari zinazotokana na ubadilishaji msimbo. Hata hivyo kuhusu sababu za ubadilishaji-msimbo kutokana na hali ya kiutambuzi, ni jambo ambalo halikuthibitishwa kikamilifu kwa sababu tulipata kuwa sio hali yenyewe pekee inayosababisha ubadilishaji-msimbo. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia kwa muhtasari kile kinachofanywa katika utafiti huu kwa kutoa mwelekeo jinsi utafiti wenyewe utakavyofanyika. Inajumuisha tatizo la utafiti, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada upeo na mipaka, yaliyoandikwa juu ya mada na nadharia, msingi wa nadharia unaojumuisha vijenzi na msingi wa nadharia, mbinu za utafiti zinazojumuisha ukusanyaji na uchanganuzi wa data na umuhimu wa utafiti. Sura ya pili imeshughulikia ubadilishaji-msimbo kwa ujumla. Imeangazia dhana yenyewe ya ubadilishajimsimbo, aina zake, dhana zinazokaribiana nao, na sababu na athari zake. Sura ya tatu na ya nne zimehusika na uchanganuzi wa data kwa kutumia vijenzi na msingi wa nadharia ya ukubalifu wa mawasiliano juu ya sababu mbalimbali za ubadilishaji-msimbo na athari zake. Sura ya tano ni hitimisho la utafiti huu pamoja na mapendekezo.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/4769
    Publisher
    University of Nairobi, Kenya
    Collections
    • Faculty of Education (FEd) [6065]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback