• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Nafasi ya mwanamke katika tenzi mbili za Shaban Robert : utenzi wa Hati na utenzi wa Adili

    Thumbnail
    Date
    2005
    Author
    Maina, Veronica
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii imeshughulikia nafasi ya mwanamke katika ushairi wa Shaaban Robert na imejikita katika tenzi zake mbili ambazo ni "Hati"na "Adili". Tasnifu hii ina sura nne. Kuna orodha ya vitabu vya marejeleo na kisha kiambatisho A-"Hati" na B - "Adili". Katika sura ya kwanza, tumeonyesha tatizo la utafiti. Aidha, tumeeleza kusudi la utafiti huu, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka ya utafiti, msingi wa kinadharia na njia za utafiti. Katika kazi hii, tumetumia tawi la nadharia ya ufeministi ambalo ni ufeministi as ilia ambalo linasisitiza uundaji wa jamii mpya ambayo itazingatia usawa wa wana kwa kuamini kuwa mabadiliko ya juujuu hayawezi kusaidia bali jamii izingatie mabadiliko ya miundo ya ndani ya kijamii. Sura ya pili inaelezea falsafa ya mshairi Shaaban Robert kuhusu maisha. Hapa tumeonyesha kuwa falsafa ya Shaaban imeathiriwa sana na dini, ukoloni na utamaduni kwa jumla. Katika sura hii, tumeanza kwa kuelezea maisha yake Shaaban. Aidha, tumeshughulikia mtazamo wake kuhusu maisha kwa kurejelea baadhi ya asasi mbalimbali za kitamaduni kama vile ndoa, dini, elimu n.k ambazo wanaufeministi wanadai kuwa huwa zinatumiwa na wanajamii ili kumdhulumu mwanamke. Katika sura ya tatu tumechunguza maudhui ya kifeministi lakini kwa kurejelea ushairi wa Shaaban tukiwa na lengo la kushughulikia nafasi ya mke katika "Hati"na "Adili". Kwa ufupi sura hii inashughulikia suala la nafasi ya mwanamke katika ushairi wa Shaaban hasa tukijikita katika "Hati"na "Adili". Sura ya nne ni hitimisho. Katika sura hii tumetoa maoni yetu kuhusu maswala tuliyoshughulikia katika tasnifu hii pamoja na mapendekezo ya kufanywa kwa utafiti zaidi.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/6283
    Publisher
    University of Nairobi, CEES, Kenya
    Subject
    Swahili poetry -- Tanzania
    Robert, Shaban
    Description
    (data migrated from the old repository)
    Collections
    • Faculty of Education (FEd) [6065]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback