• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Taswira ya jagina katika tendi: ulinganishi wa fumo liyongo na nabii isa

    Thumbnail
    View/Open
    Full-text (427.6Kb)
    Date
    2015-11
    Author
    Gathara, Francisco K
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu ulikusudia kufafanua taswira ya jagina katika utendi, kwa kumrejelea shujaa Fumo Liyongo kama alivyoelezwa katika Utenzi wa Fumo Liyongo wake Muhammed Kijumwa (1913), na Nabii Isa kama alivyoelezwa katika Utenzi wa Nabii Isa, wake Musa Mshenga (1977). Madhumuni makuu katika utafiti huu yalikuwa ni kulinganisha na kutofautisha sifa za kijagina za Nabii Isa na Fumo Liyongo, kwa nia ya kudhibitisha kuwa, sira za majagina kutoka jamii mbili zinazotofautiana katika mazingira, mila na desturi, zinaweza kufanana sana. Uchanguzi huu tuliufikia baada ya kutambua kuwa majagina wa kidini na wa kihistoria hawajatafitiwa kikamilifu. Tumeangalia historia na maisha ya Fumo Liyongo na Nabii Isa, pamoja na historia ya jamii zilizowazaa na kuwakuza, kisha tukalinganisha na kutofautisha sifa zao za kijagina kwa mujibu wa sifa bia za mashujaa. Aidha, tumeangazia umuhimu wa mashujaa hawa kwa jamii zao. Data ilikusanywa maktabani na mtandaoni, kuchanganuliwa na kubainishwa kwa msingi wa nadharia ya Uhakiki wa Vikale iliyoasisiwa na Carl Jung. Matokeo ya utafiti huu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti huu. Ilidhihirika kuwa Liyongo na Nabii Isa ni mifano mizuri ya jagina wa kihistoria na wa kidini. Mashujaa hawa pia wametokea kuwa muhimu sana katika historia ya jamii zao, na kwa ulimwengu mzima kwa jumla, na kuwa wanaweza kuwekwa katika viwango sawa na mashujaa wengine ulimwenguni. Matokeo haya vilevile yalidhihirisha kuwa, sifa za mashujaa hawa kwa kiasi kikubwa zinafanana.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/94927
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Education (FEd) [6065]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback