Maudhui ya kiukombozi katlka Diwani ya Jicho la Ndani iliyoandikwa na Said A. Mohamed

Loading...
Thumbnail Image

Date

Authors

Zani, Mwazani, E

Type

Thesis

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Nairobi

Type

Thesis

Abstract

Katika tasnifu hii tumetathmini maudhui ya kiukombozi katika diwani ya Jicha fa Ndani. iliyoandikwa na Said A. Mohamed (2002). Utafiti umeonyesha kwamba Said A. Mohamed amezingatia sana maudhui haya ya kiukombozi katika diwani hii. Hata hivyo tuligundua pia kwamba Said A. Mohamed alishughulikia maudhui mengine pia yakiwemo yale ya unyumba, siasa, dini na kadhalika. Tumeyasoma mashairi yote 96, na kugundua kwamba takriban mashairi 62 yameshughulikia mada hii ya ukombozi kwa njia moja au nyingine. Katika utafiti wetu, tumetumia nadharia ya uhalisia wa kijamii, na vigezo vyake vimetumika vilivyo katika utafiti huu. Nadharia hii iliwezesha kuhakiki maudhui ya kiukombozi kufungamana na mfumo wa jamii husika. Matokeo ya utafiti wetu yalidhihirisha kwamba mwandishi aliyashughulikia pakubwa maudhui ya kiukombozi, nia yake ikiwa ni kuwazindua wanyonge waione haja ya kujipigania waupate ukombozi.

Description

Keywords

Maudhui ya kiukombozi katlka Diwani ya Jicho la Ndani iliyoandikwa na Said A. Mohamed

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By

Creative Commons license

Except where otherwised noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States