Nafasi Ya Vijana Katika Riwaya Za Pendo La Karaha Na Kovu Moyoni

Loading...
Thumbnail Image

Date

Authors

Kihara, Isaac, S

Supervisor

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Nairobi

Type

Thesis

Abstract

Tumeangazia nafasi ya vijana katika riwaya za Pendo la Karaha na Kovu Moyoni za John Habwe. Hata hivyo ilitubidi kusoma riwaya nyinginezo za mwandishi huyu kama vile Hadaa ya Nafsi na Safari ya Lamu ili tupate ufahamu zaidi kuhusu mwelekeo wa uandishi na falsafa ya msanii huyu. Tulichagua mada ya nafasi ya vijana katika riwaya zilizohusika, kwanza kwa sababu nafasi ya vijana inaonekana kudhihirisha na kuakisi hali ilivyo katika jamii zetu. Hii ni kwa sababu jamii zetu zina mchango mkubwa katika hali ya maisha ya vijana. Tulilenga vilevile kuchunguza changamoto zinazowakabili vijana katika jamii na kuwazuia katika juhudi zao za kujikomboa kutoka katika matatizo mengi kama ukosefu wa ajira na usambazaji wa dawa za kulevya. Aidha ubinafsi, dhuluma za mapenzi kutoka kwa waajiri, unafiki wa viongozi, utabaka uliokithiri na umaskini ni baadhi tu ya changamoto wanazokumbana nazo vijana kwenye jamii. Utafiti wetu umeongozwa na nadharia ya Uhalisia Hakiki tukijikita katika kiunzi chake cha tatu kinachodai kuwa matukio au mambo yanayotendeka katika jamii hutendeka kwa kusababishwa na mambo fulani wala hayatokei tu vivi hivi. Kila tukio lina chanzo chake. Mwongozo huo umetufanya kuitathmini jamii mwanzo kabla ya kuitalii nafasi ya vijana katika riwaya zinazohusika. Kutokana na utafiti wetu, imebainika kuwa John Habwe amefaulu vilivyo katika kuwasawiri vijana na nafasi hasi na chanya wanazochukua katika jamii iliyojaa adha ya ubinafsi, uchochole, udhalimu, utabaka, na unafiki katika kutaja maovu machache. Aidha mwandishi ametoa mchango wake muhimu katika kuwajenga vijana kihadhi.

Description

Keywords

Nafasi Ya Vijana Katika Riwaya Za Pendo La Karaha Na Kovu Moyoni

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By

Creative Commons license

Except where otherwised noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States