Matumizi Ya Tashbiha, Sitiari Na Taashira Katika Damu Nyeusi Na Hadithi Nyingine

Loading...
Thumbnail Image

Date

Authors

Mwakio, Lonyce, W

Supervisor

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Nairobi

Type

Thesis

Abstract

Katika tasnifu hii tumeonyesha matumizi ya tashbiha, sitiari na tashbiha katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine ambayo ni mojawapo ya hadithi fupi za Kiswahili iliyo na hadithi kumi na tatu zilizoandikwa na waandishi mbalimbali. Katika utafiti huu, mchango wa tamathali hizi za usemi ulichunguzwa katika kuwasilisha dhamira na maudhui ya waandishi wa hadithi zilizo katika diwani hii. Ni hadithi saba kati ya kumi na tatu tulizozishughulikia ambazo tulizichagua kwa kutumia sampuli ya kusudi. Utafiti uliofanywa umekuwa wa maktabani ambapo data iliyokusanywa ilikuwa data isiyo msingi kwani tulitegemea habari zilizohifadhiwa kwenye maandishi mbalimbali. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa, waandishi wa hadithi katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine walitumia mbinu za tashbiha, istiari na taashira kwa utoshelevu na kwa njia mwafaka ili kufikia hadhira yao teule kwa njia ya kisanaa. Utafiti huu umeleta uelewa zaidi wa matumizi ya tamathali hizi kwa kazi husika.

Description

Keywords

Matumizi Ya Tashbiha, Sitiari Na Taashira Katika Damu Nyeusi Na Hadithi Nyingine

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By

Creative Commons license

Except where otherwised noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States