Mchango Wa Vijana Katika Kuleta Mabadiliko Katika Kufa Kuzikana Na Kidagaa Kimemwozea
View/ Open
Date
2017Author
Munyasya, Florence M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika utafiti huu, tumeonyesha mchango wa vijana katika kuleta mabadiliko katika riwaya za Kufa Kuzikana na Kidagaa Kimemwozea. Pia, tumeangazia changamoto ambazo vijana hukumbana nazo katika juhudi zao za kuleta mabadiliko. Utafiti wetu uliongozwa na nadharia ya uyakinifu wa kijamii ambao unajihusisha na utetezi wa wanyonge na ukombozi wao. Tumetambua kwamba vijana ni mawakala wa mabadiliko na wanaweza kuleta mchango ambao unaweza kuwafaidi wanajamii wote. Hii ni kwa sababu vijana ni wenye nguvu za mwili na maarifa ambayo wanaweza kutumia ili kuifunza jamii. Pamoja na haya, tumeonyesha kwamba vijana wanakabiliana na changamoto nyingi ambazo ni lazima zichukuliwe hatua ili kizazi hiki ambacho ni muhimu sana kipate kuokolewa. Tulitumia mbinu za utafiti za maktabani na mtandaoni. Maktabani, tulisoma riwaya mbili teule na makala tofauti kama vile tasnifu na vitabu vyenye maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa kijamii. Tulitembelea mtandao na kuangalia masuala yanayohusiana na vijana na pia tulisoma maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa kijamii.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: