Show simple item record

dc.contributor.authorMarisya, Phanice
dc.date.accessioned2017-12-14T07:14:29Z
dc.date.available2017-12-14T07:14:29Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/101893
dc.description.abstractTuliamua kuchunguza jinsi mwandishi wa riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Ndoto ya Almasi ametumia lugha ya kipekee anaporejelea masuala ya dini ya Kikristo ili kubainisha: sifa za sajili ya dini ya Kikristo zinavyojitokeza, michakato ambayo huwawezesha wafuasi wa dini ya Kikristo na wasomaji Kidagaa Kimemwozea na Ndoto ya Almasi kufasiri lugha inayohusiana na dini ya Kikristo kisha kuonyesha mchango wa matumizi ya sajili ya dini ya Kikristo katika riwaya hizi. Katika uchunguzi wetu tuliongozwa na nadharia ya pragmatiki leksika. Nadharia ya pragmatiki leksika iliasisiwa na Blutner katika mwaka wa 1990. Katika nadharia hii alionyesha jinsi maana ya neno kiisimu ilibadilishwa katika matumizi. Yaani maana ya neno hufasiriwa kulingana na muktadha fulani wa matumizi. Katika uchunguzi wetu ilibainika kuwa sifa za sajili ya dini ya Kikristo zinadhihirika katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Ndoto ya Almasi. Baadhi ya sifa hizi ni kama vile msamiati unaosifu Mungu, matumizi ya mafumbo na nyimbo za kusifu Mungu. Pia tulionyesha kuwa sajili ya dini ya Kikristo imemwezesha mwandishi wa riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Ndoto ya Almasi kufanikiwa katika kujenga maudhui, dhamira na wahusika miongoni mwa mambo mengine. Katika sura ya kwanza tumeangazia utangulizi wa kijumla kuhusu mada, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu ya kuchagua mada hii, upeo na mipaka ya utafiti wetu, maswali ya utafiti, msingi wa kinadharia na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili tumeonyesha udhihirikaji wa wa sajili ya dini ya Kikristo katika matini husika. Aidha, tumeshughulikia uchanganuzi wa semi za dini ya Kikristo katika sura ya tatu huku tukiegemea kwenye kategoria za kimsingi zilizofafanuliwa na Wilson (2003) na Cartson (2002) katika nadharia ya pragmatiki leksika. Sura ya nne inahusu umuhimu wa sajili ya dini ya Kikristo katika riwaya husika. Hatimaye tumehitimisha kazi hii na kutoa mapendekezo yetu katika sura ya tano.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMchango Wa Sajili Ya Kidini Katika Kufanikisha Riwaya Mbili Za Ken Walibora (Kidagaa Kimemwozea Na Ndoto Ya Almasi)en_US
dc.titleMchango Wa Sajili Ya Kidini Katika Kufanikisha Riwaya Mbili Za Ken Walibora (Kidagaa Kimemwozea Na Ndoto Ya Almasi)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States