Matumizi Ya Lugha Katika Maulidi Ya Jambezi
Abstract
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya na kuniwezesha kukamilisha kazi hii kwa wakati ufaao. Vilevile nawashukuru wasimamizi wangu Profesa Abdulaziz Mohammed, Profesa Kinene wa Mutiso na Profesa Rayya Timammy kwa kunipa mwongozo thabiti na motisha katika kipindi hiki. Walinifaa sana katika kuisoma na kuirekebisha kazi hii hata ikakamilika. Mola awape afya njema na maisha marefu ili waendelee kuwaongoza wanafunzi wengine siku za usoni.
Shukrani nyingine ni kwa wahadhiri wafuatao katika idara ya Kiswahili, chuo kikuu cha Nairobi. Prof. Iribe Mwangi, Prof. John Habwe, Prof. Mwenda Mbatia, Dkt. Zaja Omboga, Dkt. Jefwa Mweri, Dkt. Evans Mbuthia, Dkt. Prisca Jerono na Bwana Leonard Sanja. Waliniongoza katika kila hatua ya safari hii ya usomi na hata katika kufanya utafiti huu. Mola awabariki.
Shukrani zangu za dhati pia ziwaendee wanafunzi wenzangu tulioanza nao safari hii ya usomi kwa kuhimizana na kutiana motisha katika hali zote. Baadhi ya wanafunzi hawa ni: Ray, Florence, Lilian na Muinde. Nawatakia kila la kheri.
Pia namshukuru mume wangu, Bw. Mwachizi Mwero kwa msaada wake wa hali na mali wakati wa kipindi hiki cha usomi. Mungu ambariki sana. Sitawasahau watoto wangu: Allan, Michael na Moses kwa kunitia moyo na kunivumilia wakati wote wa masomo haya. Rabbana awahifadhi.
Mwisho namshukuru mwalimu mkuu Bw. Daniel Karanja pamoja na walimu wenzangu. Walinisaidia sana kwa kusimamia shughuli zilizohitaji uelekezi wangu nilipokuwa nikifanya utafiti huu. Mungu awatimizie haja za mioyo yao. Nitakuwa mtovu wa nidhamu kama sitamshukuru Bw. Wanga aliyepiga chapa kazi hii kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mola abariki kazi ya mikono yake.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Matumizi Ya LughaRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: