dc.description.abstract | Mada yetu ina sura nne, ambazo zinaingilia mambo mbali
mbali~katika sura ya kwanza, tunajishughulisha na
methodolojia ambayo tuliitumia katika utafiti wetu.
Katika sura hii hii tumeeleza nadharia tuliyoiteua, udurusu
wa vitabu, haipothesia na kadhalika.
Katika sura ya pili tumejishughulisha na Malenga wa
Vumba(1982), ambapo tumeingilia maudhui mbali mbali, ambayo
yamejadiliwa katika diwani hiyo.
Katika sura ya Tatu tumeingilia riwaya ya Zablbu Chungu(1985)
na kuchunguza maudhui pamoja na wahusika.
Na mwisho katika Sura ya nne, tumehitimisha kazi yetu
kwa kuchunguza picha jumlishi ya mwandishi, kama
inavyojitokeza katika maandishi tuliyoyataja. | en_US |