Show simple item record

dc.contributor.authorBarasa, Reuben W
dc.date.accessioned2019-01-15T12:33:14Z
dc.date.available2019-01-15T12:33:14Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/104768
dc.description.abstractTasnifu hii imetafiti mielekeo ya wanafunzi na wadau wengine katika shule ya sekondari ya Jamhuri jijini Nairobi kuhusu lugha kipindi ya Sheng. Kazi hii imelenga hasa kubaini iwapowanafunzi na wadau wengine wa shule ya upili ya Jamhuri wanaenzi lugha ya Sheng kuliko lugha zingine wanazozifahamu, kutambua miktadha ambamolugha ya Sheng hutumiwa katika shughuli zao za kimawasiliano na pia, kutathmini mitazamo na mielekeo ya wazazi na walimu wa wanafunzi kuhusu matumizi ya lugha ya Sheng na wanafunzi wa shule hii na vile vile kutafiti mchango wa wafanyikazi wasio walimu na wadau wengine katika shule ya upili ya Jamhuri kuhusiana na matumizi ya lugha ya Sheng miongoni mwa wanafunzi.Ili kutimiza malengo haya, utafiti huu umetumia nadharia ya kisaikolojia ya jamii ili kuweza kufanikasha malengo yetu. Sampuli iliyotumika kwa kupata data ya utafiti huu ilihusu jumuiya nzima ya shule ya upili ya Jamhuri jijini Nairobi. Uteuzi huu umefanywa kimaksudi. Mbinu zilizotumika katika kupata data ya kazi hii ilihusu matumizi ya hojaji na vile vile mahojiano mbali na kusoma katika maktaba hasaa kuhusu swala zima la Sheng na nadharia iliyotumika katika utafiti huu umebaini kuwa; wanafunzi na wadau wengine wa shule ya upili ya Jamhuri wanaenzi lugha ya Sheng kuliko lugha zingine wanazozifahamu kutokana na mielekeo yao kuhusu Sheng, miktadha ambamo wanafunzi na wadau wengine wa shule ya upili ya Jamhuri hutumia lugha ya Sheng katika shughuli zao za kimawasiliano imedhihirikakuwa ni shuleni, nyumbani, sehemu za burudani na hata sokoni, mitazamo na mielekeo nayo ya wazazi na walimu wa wanafunzi na wadau wengine wa shule ya upili ya Jamhuri kuhusu matumizi ya lugha ya Sheng na wanafunzi wa shule hii ilikuwa chanya kutokana na mielekeo yao na pia mchango wa wafanyikazi wasio walimu na wadau wengine kuhusiana na matumizi ya lugha ya Sheng miongoni mwa wanafunzi ulikuwa mkubwa kutokana na mielekeo yao chanya kuhusiana na lugha ya Sheng. Sababu kuu ya kuchangamkia Sheng ni kuwa inatumiwa na vijana na wazee vijana wa jinsia zote kufumbia mambo na kwa hiyo kuifanya kuwa lugha ya kundi ndani. iven_US
dc.language.isoothersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMielekeo Ya Wanafunzi Na Wadau Wengine Wa Shule Za Sekondari Kuhusu Sheng: Kifani Cha Shule Ya Upili Ya Jamhuri, Nairobien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States