Show simple item record

dc.contributor.authorMturo, Neema G
dc.date.accessioned2019-01-17T06:34:16Z
dc.date.available2019-01-17T06:34:16Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/104901
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu jiniuchawi na ushirikina kama mikakati ya uchimuzi katika riwaya za kimajaribio za Maundu Mwingizi za Vita vya Mapenzi (2012), Mzimu wa Waufi (2013) na Tanzia (2015). Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuonyesha jinsi mandhari za kijiniuchawi na kishirikina zinavyotumiwa kimkakati kuchimuza dhamira na maudhui mbalimbali, hali kadhalika zinavyotumiwa katika usawiri na uchimuzi wa wahusika wa kijiniuchawi na kishirikina katika riwaya za Mwingizi. Madhumuni mengine ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha jinsi ishara na uashiriaji zinavyotumiwa kama mikakati ya uchimuzi katika riwaya za Mwingizi. Ili kufanikisha utafiti huu, nadharia mbili zimetumika—nadharia ya uhalisiajabu na nadharia ya Semiotiki. Nadharia ya uhalisiajabu imetumika zaidi katika utafiti huu kwani riwaya zilizochanganuliwa katika utafiti huu zimekitwa zaidi katika maswala ya kihalisiamazingaombwe. Kwa upande wa Semiotiki, nadharia hii imetumika zaidi katika sura ya tano kwani sura hii imejikita zaidi katika kuangalia ishara. Kwa hiyo, nadharia hii imesaidiana na nadharia ya uhalisaiajabu katika kufanikisha utafiti huu mpaka ukakamilika. Utafiti huu kwa kiasi kikubwa umekuwa ni wa maktabani uliohusisha usomaji, uchanganuzi na utathimini wa riwaya za Vita vya Mapenzi (2012), Mzimu wa Waufi (2013) na Tanzia (2015) za Maundu Mwingizi na ndizo zilizotupa data ya msingi. Uchakataji wa data umeongozwa na makabala wa kitaamuli. Kwa jumla, matokeo ya uchanganuzi wa data kutoka katika riwaya hizi yameweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yamebainisha mandhari, wahusika na ishara za kijiniuchawi na ushirikina zimeweza kuchimuza maudhui mbalimbali kama ya uongozi wa kiimla, mauaji na ufadhili wa kisiasa, mahusiano kati ya wahalifu na vigogo serikalini, ung’ang’aniaji madaraka na urithishanaji uongozi, uhuru wa bendera na ukoloni mamboleo, unafiki, uongo, mikataba ya kilaghai, utandawazi, usaliti, maadili, haki na sheria, ukatili, mafao binafsi, uwajibikaji, mifumo ya kiutawala, unyonyaji, malezi, mapenzi, pesa, nafasi ya mwanamke, familia, uaminifu, utii, migongano katika dini, heshima, utamaduni, misukosuko ya kindoa na mahusiano ya kifamilia, unyenyekevu, mitandao ya jinai katika jamii, mali ya umma, dhuluma dhidi ya wanawake na utawala kandamizi. Utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kitaaluma katika uwanja wa fasihi ya Kiswahili katika kuonyesha kwamba riwaya za kihalisiajabu zimeimarika zaidi katika kutumia dhana za jini uchawi na ushirikina kama ufundi au mtindo wa kifani.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleJiniuchawi Na Ushirikina Kama Mkakati Wa Uchimuzi Katika Riwaya Teule Za Maundu Mwingizien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States