Show simple item record

dc.contributor.authorWangeci, Wanjiru Agnes
dc.date.accessioned2019-01-23T11:19:40Z
dc.date.available2019-01-23T11:19:40Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105345
dc.description.abstractUtafiti wetu ulilenga kuonyesha ukiushi wa kiisimu katika jumbe cheshi za mtandao katika viwango sita ambavyo ni kiwango cha kigrafolojia, kilekska, kimofolojia, kisintaksia, kisajili na pia kisemantiki. Kwa kuonyesha ukiushi wa kiisimu katika jumbe cheshi, tulilenga kupinga kwa njia moja fikra kuzihusu jumbe cheshi kuwa zinajitokeza na makosa ya aina mbalimbali kama vile ya kisarufi. Kwa hivyo, tulidhibitisha katika utafiti wetu kuwa ukiushi wa kiisimu haujajitokeza kimakosa bali ni tukio la kimakusudi linalolenga kuongezea mvuto wa kiusanii kwenye akili ya msomaji ujumbe. Tuliongozwa na nadharia mbili ambazo ni nadharia ya semiotiki inayohusu ishara za lugha na pia nadharia ya elimumitindo inayohusu ufafanuzi wa kiisimu kuhusu mitindo mbalimbali inayojitokeza katika matini mbalimbali za kisanii. Jumbe cheshi ambazo ndizo data ya uchunguzi zimesakuriwa kutoka kwa wavuti mbalimbali na husambazwa kupitia mtandao kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Jumbe cheshi hizi zilichanganuliwa na matokeo yake yalirekodiwa katika sura ya tatu na ya nne. Idadi ya jumbe cheshi 49 zilitumika kama data ya uchunguzi. Matokeo ya utafiti yalidhibitisha ukiushi wa kiisimu wa jumbe cheshi za mtandao katika viwango vilivyotajwa.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUkiushi Wa Kiisimu Katika Jumbe Cheshi Za Mtandaoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States