Show simple item record

dc.contributor.authorOyaro, Christine
dc.date.accessioned2020-02-24T12:33:57Z
dc.date.available2020-02-24T12:33:57Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/108428
dc.description.abstractTafsiri za methali na misemo katika kazi za fasihi, hasa fani hizi zinapotokea kuwa na uamilifu wa kipekee katika kazi husika huhitaji kutafsiriwa kwa njia ambayo itafanikisha dhamira ya mwandishi kuhusiana na matumizi ya fani hizo. Mtafsiri huhitajika kutambua kuwa methali na misemo, mbali na jukumu la kupamba lugha ili kuifanya ivutie na kupitisha ujumbe maalum, wakati mwingine hutumika kama viungo vya kimsingi katika kuchimuza maudhui na kuisukuma mbele hadithi. Hali kama hii inajitokeza katika Arrow of God ambapo methali na misemo imetumika kufanikisha dhamira ya mwandishi, Chinua Achebe. Inabainika kwamba methali na misemo miongoni mwa vifani vingine vya fasihi simulizi ya watu wa jamii ya Igbo imetumiwa na Achebe ili kubadilisha lugha ya Kiingereza kuchukua sifa za kitamaduni za jamii ya Igbo. Katika tasnifu hii tafsiri za methali na misemo, kama zilivyofanywa na Hafid Shamte (1974), zimechunguzwa ili kutathmini mbinu alizotumia kutafsiri na kubainisha kama zinatimiza lengo la matumizi ya fani hizi katika Arrow of God baada ya kutafsiriwa kwa Kiswahili katika Mshale wa Mungu.Inabainika kuwa Shamte anatumia mbinu mbali mbali kutafsiri methali na misemo kutoka Arrow of God hadi Mshale wa Mungu. Miongoni mwa mbinu hizi, mbinu ya uhawilishaji inajitokeza kwa kiwango kikubwa. Matokeo ya tafsiri zinazotokana na mbinu hizi ni kwamba methali na misemo imejitokeza ama kama kama maelezo tu, au wakati mwingine vipengee vya utamaduni aliokusudia kuwasilisha Achebe vimepotea katika mchakato wa tafsiri. Hali hii inapelekea mapendekezo ya kufanya tafsiri kwa kutumia mbinu ambazo kwa kadri iwezekanavyo, zitadumisha sio tu mtindo wa methali, bali pia ujumbe wa mwandishi kwa njia inayosawazisha tamaduni mbili; utamaduni wa lugha chanzi na ule wa lugha lengwa.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectTafsiri za Methali na Misemo katika Mshale wa Munguen_US
dc.titleTafsiri za Methali na Misemo katika Mshale wa Munguen_US
dc.typeThesisen_US
dc.contributor.supervisorTIMAMMY, RAYYA
dc.contributor.supervisorZAJA, OMBOGA .J.


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States