Show simple item record

dc.contributor.authorAsiko, Anne Fl
dc.date.accessioned2020-02-25T12:45:58Z
dc.date.available2020-02-25T12:45:58Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/108463
dc.description.abstractShukrani zangu natoa kwa wahusika mbalimbali ambao kama hawangekuwa kazi hii haingefikia kilele hiki. Ninaanza kwa kumshukuru Maulana ambaye neema zake zinatosha. Alinibariki kwa fikira, fedha, wakati na kuniweka karibu na waja waliotia juhudi zao kunisaidia kukamilisha kazi hii. Shukrani za pili nawapa Dkt. Omboga Zaja na Dkt. Samuel Obuchi ambao walichukua muda wao kusoma kazi yangu na kunielekeza kila mara bila kuchoka. Mwanzoni pia nilifanya kazi na Dkt. Ayub Mukhwana ambaye wasia wake hauwezi ukasahaulika. Tajriba ya Dkt. Omboga Zaja na uzoefu wa Dkt. Obuchi umedhihirika katika kazi hii. Rabana awape neema zake ili muendelee kutoa wasomi wengine zaidi. Shukrani zangu nyingine ziwaendee wahadhiri wangu wote walionifunza kozi za uzamili kwa bidii, ukakamavu na ujuzi wa hali ya juu. Sitawahi kuwasahau; Prof. Iribe Mwangi kwa mawaidha yake ya kila mara, Prof. John Habwe kwa maoni yake yenye manufaa hapo mwanzoni mwa tasnifu hii. Wahadhiri wa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Nairobi ambao pia wanastahili pongezi kwa mafunzo yao yenye hekima ni pamoja na Prof. Kineene wa Mutiso, Prof. Mwenda Mbatia, Dkt. Prisca Jerono, Dkt. Omboga Zaja, Dkt. Jefwa Mweri, Dkt. Amiri Swaleh na Prof. Evans Mbuthia. Wenzangu wa darasa la uzamili pia wana nafasi ya kipekee katika moyo wangu. Hawa ni pamoja na Lilian, Sylveria, Agnes, Asha, Adeline, Carolyne, Flora, Winfred, Jackline, Wangeci, Bi. Gitonga, Nyambeki, Kemunto, Emily, Bosibori, Njeri, Polycarp, Chesebe, Misheck, John Bosco, Kevin, Mengistu, Saar, Jared, Mogusu, Mwangi na Roy. Kwa sababu ya ucheshi, uwazi na bidii zenyu za mchwa, mlikuwa washirika wazuri sana, kozi ikaonekana nyepesi. Shukrani hizi natoa kwa wataalam waliokuwa tayari kunijibu kila mara nilipokuwa na swali kuhusu istilahi za elimumisitu, Melvin Ouma kutoka Nakuru, Rosemary Gastor Sabida kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Huduma ya Misitu, Tanzania na Vuai Mkoko Hassan kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili, Idara ya Misitu na Rasilimali Zisizoejesheka, Zanzibar. Ninawashukuru wazazi wangu, hasa marehemu babangu Mzee Antony Ogutu Asiko, ambaye kwa uthabiti wake alihakikisha amewekeza kwa elimu yangu. Bila bidii zake, utunzaji wa mamangu na v ushauri wa ami yangu Mzee Elijah Obare Asiko singekua hadi kiwango hiki. Siwezi nikamsahau bavyaa yangu Mzee Jacob Mukolwe kwani alithamini maendeleo yanayohusu masomo. Nafasi hii naipa familia yangu, mume wangu mpendwa Michael na wanangu Marion, Stephen na marehemu Fabian, wanastahili shukrani za dhati kwa kuniruhusu nirudi masomoni, kuhudhuria mihadhara, kudurusu kwa muda mrefu na kutumia fedha kwa shughuli hizi. Ilibidi mjitolee mhanga ili kazi hii ifikie hatima yake. Mola awabariki. Mwisho ni shukrani kwa walimu wenzangu; Bw. Hippolitus Omondi, mwalimu mkuu, kwa kunipa idhini ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Nairobi mara kwa mara, Bw. Francis Malowa na Charles Otieno ambao walichangia kwa kupiga chapa na kutoa tasnifu hii. Ninawashukuru walimu wa Idara ya Lugha, hasa Kiswahili, Binti Carolyne Ochola na Esther Oduor, walioshikilia sehemu ya kazi niliyostahili kufanya nilipoondoka. Walimu wote wa Shule ya Upili ya Ndenga wanastahili shukrani kwa usaidizi wowote waliotoa. Kama nimemsahau mtu yeyote aniwie radhi, nina shukrani tele moyoni kwa kufikia mwisho wa utafiti huu.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity Of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUtunzaji Wa Miti Katika Misituen_US
dc.titleUshawishi Wa Kiasi Cha Habari Kinachopitishwa Katika Tafsirien_US
dc.typeThesisen_US
dc.contributor.supervisorOmbogo, Zaja
dc.contributor.supervisorObuchi, S.M


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States