Show simple item record

dc.contributor.authorGatere, Lucy N
dc.date.accessioned2020-02-27T09:10:15Z
dc.date.available2020-02-27T09:10:15Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/108647
dc.description.abstractMada ya utafiti huu ilikuwa kuchunguza usawiri wa familia ya kisasa katika fasihi ya watoto nchini Kenya. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha aina za familia zinazosawiriwa katika fasihi ya watoto, kutathmini usawiri wa familia kama taasisi katika fasihi ya watoto na kuchunguza uhalisi wa kifamilia unavyoakisika katika hadithi za watoto. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia wa kijamii ambayo ilitoa msingi madhubuti wa kutathiminia usawiri wa familia ya kisasa kwa vile imethibitika kuwa usawiri unaobainika unafungamana na hali ilivyo katika maisha ya jamii ya kisasa. Utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo na ulikuwa wa maktabani. Vitabu vilivyoteuliwa vilisomwa kwa makini na data inayohusu usawiri wa familia kuchukuliwa kwa kujibu maswali ya utafiti. Vitabu vilivyoteuliwa kwa utafiti huu vilikuwa katika migao miwili; vitabu vya hadithi za watoto vilivyotungwa kati ya 2000 hadi 2010 ambavyo ni Mwepesi wa Kusahau, Nampenda Mama wa Kambo na Madalala Abadilika na vitabu vya hadithi za watoto vilivyotungwa kati ya 2011 hadi 2018 ambavyo ni Cheupe na Cheusi, Likizo ya Mkosi na Ahaa! Roda. Mgao huu wa kiuteuzi ulilenga kuangalia ni kwa jinsi gani tungo hizi zinaakisi uhalisi wa wakati katika kusawiri familia. Baada ya kuvisoma vitabu vilivyoteuliwa, muhtasari wa kila hadithi ulitolewa na data kudondolewa kwa kuzingatia madhumuni na maswali ya utafiti huku maelezo yakitolewa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo na hatimaye matokeo na mapendekezo kuwasilishwa. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa aina za familia zimebaki kuwa zilezile hata vipindi vya kiwakati vinapobadilika. Aina hizo ni familia kiini na familia pana. Kuhusu usawiri wa familia, utafiti huu, ulibainisha kuwa katika kipindi cha awali familia ilisawiriwa kama ambayo inashughulikiwa na mama zaidi ya baba kuhusu malezi ya watoto. Hali hii inaendelea kubadilika katika kipindi cha sasa ambapo baba katika familia anasawiriwa kama anayeshughulikia majukumu yake vilivyo. Kwa mtazamo wa nadharia ya uhalisia, usawiri huu ulionekana kuwa na uhusiano mkubwa na familia halisi katika jamii. Kutokana na matokeo ya utafiti huu inapendekezwa kuwa usomaji wa fasihi ya watoto shuleni usiwe wa burudani tu lakini utilie mkazo ujenzi wa mitazamo chanya miongoni mwa watoto wakiwa wangali wadogo kuhusiana na usawiri wa familia. Makuzi ya watoto na ufunzaji wa maadili ni mambo yawezekanayo sio katika misingi ya familia tu bali pia kupitia mafunzo ya fasihi ya watoto. Aidha, inapendekezwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu usawiri wa familia katika nyakati za awali kabisa.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectFasihi Ya Watoto Nchinien_US
dc.titleUsawiri Wa Familia Ya Kisasa Katika Fasihi Ya Watoto Nchini Kenyaen_US
dc.typeThesisen_US
dc.contributor.supervisorTimmamy, Rayya
dc.contributor.supervisorOmbaga, Zaja


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States