Show simple item record

dc.contributor.authorKimwea, James G
dc.date.accessioned2020-03-04T09:05:16Z
dc.date.available2020-03-04T09:05:16Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/108840
dc.description.abstractKwa namna ya kulinganisha na kulinganua, tasnifu hii imechunguza taswira ya jamii katika riwaya ya Yasinya (2014) ya Leonard Sanja Leo na Mwanasiasa (2014) ya Swale Mdoe. Tatizo la utafiti wetu limekuwa kuhakiki maudhui ya mgawanyiko wa jamii kitabaka katika riwaya hizo kwa msingi wa nadharia ya u-Marx wa kirasimi. Uchunguzi wetu katika tafiti za awali kuhusu uhakiki wa maudhui katika riwaya umeonyesha kwamba maudhui hayo — japo ndiyo yanayosisitizwa katika nadharia inayohusika — hayajashughulikiwa katika riwaya teule. Lengo letu la kwanza limekuwa kuhakiki maudhui, kutathmini uhalisia wake na kuonyesha kiasi cha kuhusiana kwa maudhui katika Yasinya na Mwanasiasa na suala la mgawanyiko wa jamii kitabaka. Lengo la pili limekuwa kubainisha jinsi fani kwa jumla ilivyotumiwa kuwasilisha maudhui ya mgawanyiko wa jamii kitabaka katika riwaya teule.Kazi yenyewe ina sura nne.Sura ya kwanza ina utangulizi, tatizo la utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, umuhimu wa utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada, misingi ya nadharia, haipothesia na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili, tumehakiki maudhui, tukatathmini uhalisia wake na kuonyesha kiasi cha kuhusiana kwa maudhui hayo na suala la mgawanyiko wa jamii kitabaka. Sura ya tatu imebainisha jinsi fani — kwa jumla — ilivyotumiwa kuwasilisha maudhui ya mgawanyiko wa jamii kitabaka katika riwaya za Yasinya na Mwanasiasa. Sura ya nne ina hitimisho la utafiti ambapo tumetoa maelezo ya kina kuhusiana na malengo ya utafiti. Aidha, tumechunguza ufaafu wa nadharia ya u-Marx wa kirasimi na changamoto za utafiti. Mwisho kabisa, tumetoa pendekezo kuhusu utafiti wa baadaye, tukaweka muhtasari wa hitimisho na orodha ya marejeleo.Kwa ufupi, matokeo ya utafiiti huu yamekuwa kwamba maudhui makuu ya mgawanyiko wa jamii kitabaka ni umaskini na utajiri. Maudhui hayo yamewasilishwa kiuhalisia japo kuna ukwepaji wa uhalisia kwa viwango tofauti katika riwaya teule. Ni kupitia kwake ambapo matabaka makuu katika jamii yamesawiriwa. Tabaka la matajiri ni la watawala, ukoo na washirika wao huku la maskini likiwa la watawaliwa. Kwa hivyo, matabaka makuu katika jamii ya sasa hayakusawiriwa kama Marx alivyoyaeleza.Hivi ni kutokana na mfumo wa kiuchumi, ulio ubepari uchwara, unaoendelezwa katika jamii zinazowakilishwa na riwaya tulizozihakiki na ambao ndio pia unaotawala mataifa ya Kiafrika kwa sasa. Katika mfumo huo, matabaka aliyoyazungumzia Marx (mabwanyenye na wafanyikazi) na yaliyokuwa na dhima ya kuzua mivutano ili kuiwezesha jamii kuendelea na kufikia ukamilifu wa kinjozi kupitia ngazi za kiuchumi: ujima, utumwa, umwinyi, ubepari, ujamaa na kisha ukomunisti hayapo. Kwa mujibu wa riwaya teule, mivutano iliyopo katika jamii ni baina ya tabaka tawala na tabaka tawaliwa. Hata hivyo, nafasi ya mivutano hiyo kuleta maendeleo chanya ya jamii ni finyu mno hasa katika riwaya ya Yasinya.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity Of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectTaswira Ya Jamiien_US
dc.titleTaswira Ya Jamii Katika Riwaya Za Yasinya Na Mwanasiasaen_US
dc.contributor.supervisorMwenda, Mbatiah
dc.contributor.supervisorGitonga, Joseph


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States