Show simple item record

dc.contributor.authorMariga, Edward
dc.date.accessioned2020-05-20T06:05:14Z
dc.date.available2020-05-20T06:05:14Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/109687
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza kutojitokeza kwa lugha ya kitamathali na urejeleaji wa kijinsia katika Wimbo Ulio Bora kama matini lengwa, matini hii inapolinganishwa na matini chanzi Song of Songs. Kitabu hiki ni cha ishirini na mbili katika agano la kale kwa mujibu wa tafsiri ya King James Version. Katika utafiti huu, tamathali tulizojikita kwazo ni pamoja na tashbihi, sitiari pamoja na tashihisi. Tulibainisha tamathali hizi katika matini chanzi na vilevile jinsi ambavyo tamathali hizi zilivyohawilishwa katika matini lengwa. Jambo lingine ambalo tuliliangazia ni lugha inayorejelea jinsia ya kiume na ya kike katika matini chasili huku tukilinganisha na matini lengwa kwa lengo la kubaini ulinganifu katika kujitokeza kwa urejeleaji huo wa kijinsia. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Newmark (1988) ya tafsiri ya masuala mahususi ya kitamaduni. Tuliangalia makundi matano ya masuala mahususi ya kitamaduni yanayopendekezwa na nadharia hii. Pamoja na kufanya hivi, tulichunguza jinsi masuala haya mahususi yanavyojitokeza katika matini lengwa kwa kuilinganisha matini hiyo na matini chasili. Utafiti tulioufanya ulikuwa wa maktabani kwa kuwa data tuliyokusanya ilikuwa data isiyo msingi ambapo tulitegemea habari zilizohifadhiwa kwa njia ya maandishi katika bibilia ya Kiingereza (tafsiri ya King James) na tafsiri yake katika lugha ya Kiswahili (Swahili Union Version). Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha masuala mbalimbali ya kitafsiri. Kwanza ni kwamba, lugha ya Kiingereza kupitia matini chanzi Song of Songs inadhihirisha urejeleaji wa kijinsia. Urejeleaji huu umejitokeza katika vitengo mbalimbali kama vile nomino, virai nomino, vivumishi pamoja na viwakilishi. Lugha ya Kiswahili kupitia kwa matini chanzi Wimbo Ulio Bora hata hivyo, inadhihirisha kwa kiasi kidogo tu urejeleaji huu wa kijinsia. Aidha utafiti huu vilevile ulizichunguza tamathali tatu husika (tashihisi, tashbihi na sitiari) kwa kutathmini kujitokeza kwa tamathali hizi katika matini lengwa ambapo matokea yalionyesha kuwa tamathali hizi zimekosa ulinganifu kwa kiasi kikubwa matini mbili husika zinapolinganishwa. Aidha, tulitafitia masuala mahususi ya kitamaduni kwa kuyagawa katika makundi yake matano kama anavyopenekeza Newmark (1988) na kisha kuchunguza mikakati iliyotumika katika kuyahawilisha masuala haya hadi lugha lengwa. Utafiti huu umebainisha kwamba kutojitokeza kwa lugha inayorejelea jinsia, ukosefu wa ulinganifu wa kitamathali na kidhana kunatokana na tofauti kati ya lugha mbili husika ambapo tamaduni zinazoambatana na lugha husika (Kiswahili na Kiingereza) zinadhihirisha mielekeo tofauti katika kuyadhihirisha masuala ya kijinsia, kitamathali na kidhana.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectLugha Ya Kitamathalien_US
dc.titleKutojitokeza Kwa Lugha Ya Kitamathali Na Urejeleaji Wa Kijinsia Katika Wimbo Ulio Boraen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States