Show simple item record

dc.contributor.authorNaliaka, Ruth
dc.date.accessioned2013-02-26T08:00:32Z
dc.date.available2013-02-26T08:00:32Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/11527
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia uhakiki wa hali ya vijana katika Vipanya rya Maabara kwa kuegemea maudhui na wahusika. Katika sura ya kwanza, tumeangazia Somo la Utafiti, Madhumuni, Nadharia Tete, Sababu za kuichagua mada hii, Yaliyoandikwa kuhusu mada yenyewe, Msingi wa kinadharia pamoja na njia za utafiti. Sehemu hii kwa haltika ni kama msingi wa kazi yetu ya utafiti tulioufanya. Katika sura ya pili tumejadili dhana ya uhusika kwa jumla. Tumeangalia aina mbali mbali za wahusika kama wanavyoainishwa na wataalam mbali mbali huku tukibainisha mwiingiliano mkubwa uliopo baina ya makundi hayo tofauti tofauti. Sura yenyewe ina umuhimu mkubwa katika kuwaelewa wahusika pamoja na usawiri na umuhimu wao katika kazi ya fasihi. Sura ya tatu imeshughulikia wahusika. Katika sehemu hii, tumewachambua wahusika kwa kuangazia aina zao, usawiri wao pamoja na umuhuimu wao. Sifa zao mbali mbali vile vile zimejadiliwa. Hata hivyo umuhimu mkubwa zaidi umepewa vijana kwa kuonyesha jinsi gani wanavyotumiwa kama vipanya vya maabara pamoja na matatizo mbali mbali zinzowakumba. Sura ya nne imeshughulikia maudhui huku uzito ukipewa matatizo yanayowakumba vijana katika sehemu za mijini nchini Kenya ingawa mji wa Nairobi umetumiwa kama mandhari ya riwaya hiyo. Mbali na matatizo, kunao vile vile ujumbe chanya ambao umeangaziwa kuwahusu vijana Kwa vile vijana hawawezi kupatikana katika jamii isyo na wazee, kundi hili la watu wakomavu pia limehusishwa katika maudhui kwa sababu matatizo mengi yanayowakumba vijana yanasababishwa ama na wazazi au watu wengine wazima wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Sura ya tano imebeba hitimisho la utafiti wetu kwa lengo la kudhibitisha ufanisi kwa utafiti wenyewe kwa mujibu wa madhumini na nadharia tete zetu. Tumebainisha matokeo ya utafiti pamoja na matatizo yaliyotukabili wakati wa kufanya utafiti huu. Hatimaye tumetoa mapendekezo kuhusu utafiti unaoweza kufanywa baadaye kuhusiana na kazi kama hii.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUhakiki wa hali ya vijana katika riwaya ya Vipanya vya Maabaraen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record