Show simple item record

dc.contributor.authorOtwere, Samson
dc.date.accessioned2013-02-26T08:00:34Z
dc.date.available2013-02-26T08:00:34Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/11533
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu usonde katika tafsiri tathmini ya tafsiri za Makala ya Adult Sabbath school Bible Study Guide.Glimpses of our God January, February and March na Mafundisho ya Biblia katika Shule ya Sabato kwa Watu Wazima miezi ya Januari, Februari na Machi 2012.'Tasnifu hii inalenga kutathimini usonde kama kipengele kimojawapo kinachoathiri maana. Uelewa wa matumizi ya usonde huleta ulinganifu wa maana baina ya makala asilia na makala pokezi. Utafiti uliofanywa mbeleni umeshughulikia masuaia ya kisintakisia Kaviti (2005), matatizo ya tafsiri katika vyombo vya habari Ali (1981), ulinganifu katika tafsiri za kifasihi Nyaga (2009) na kushughulikia kipengele cha umaanisho cha pragmatiki kwa kutumia nadharia ya muwala Simiyu (2010). Usonde kama kipengele cha pragmatiki ni muhimu katika tafsiri kwa sababu kinashughulikia muktadha. Maneno ya usonde hushirikisha muktadha iIi kupata maana. Mtafsiri anastahili kukitilia maanani kipengele cha muktadha iIi aweze kutafsiri inavyostahili iIi kuepuka kutoa maana tata au potovu katika tafsiri. Tasnifu hii imegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi unaofafanua maana ya usonde na nafasi ya usonde katika kujenga ulinganifu wa maana katika kukuza mawasiliano katika tafsiri. Tutaangazia aina za usonde zinazojitokeza katika makala najinsi usonde huathiri ulinganifu katika kiwango cha mawasiliano. Pia tutaonyesha tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kulichagua somo hili, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu somo, msingi wa kinadharia tulioutumia, njia za utafiti na umuhimu wa utafiti huu. Katika sura ya pili tutaeleza aina mbalimbali za usonde. Tutaeleza jinsi usonde huchangia katika kujenga ulinganifu wa ujumbe katika Me na ML. Tutamlika matatizo yanayoweza kutokea wakati wa kutafsiri vipengele hivi na kuonyesha umuhimu wa usonde katika tafsiri. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa makala ya Adult Sabbath school Bible Study Guide: Glimpses of our God na Mafundisho ya Biblia katika Shule ya Sabato Kwa watu wazima: Mionekano ya Mungu Wetu, kutumia nadharia ya umaanisho ya Grice. Katika utafiti huu tutaonyesha jinsi usonde umeshughulikiwa na kuonyesha matatizo yanayomkabili mtafsiri katika kuhamisha maana kutoka matini chanzi hadi matini pokezi. Sura ya nne imeshughulikia uchanganuzi wa data, tathmini ya madhumuni na nadharia tete, ufaafu wa wa nadharia tuliyoitumia, changamoto tulizokumbana nazo katika utafiti huu na hatimaye hitimisho na mapendekezo ya utafiti mpya.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUsonde katika tafsiri: Tathmini ya mafundisho ya Biblia katika shule ya Sabato kwa watu wazimaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record