Show simple item record

dc.contributor.authorWere, Everlyne
dc.date.accessioned2013-02-26T08:00:35Z
dc.date.available2013-02-26T08:00:35Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/11539
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza fani katika tamthilia ya Kiswahili. Tamthilia zilizoteuliwa kuhakikiwa katika kazi hii ni mbili; Kilio cha Haki (1981) na Kijiba cha Mayo (2009). Sura ya kwanza ni msingi wa utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchangua mada, upeo na mipaka ya utafiti na msingi wa nadharia. Pia, imejumuisha udurusu wa yaliyoandikwa kuhusu mada na njia au mbinu za utafiti zilizotumika katika kazi hii. Sura ya pili imeshughulikia dayolojia na monolojia katika tamthilia tulizoziteua. Tumeangazia dhana ya vipengele hivi na umuhimu wa vipengele hivi katika kazi hizi kwa kutolea mifano mwafaka. Sura ya tatu imeangazia upambanuzi wa wahusika katika Kilio cha Haki na Kijiba cha Mayo. Tumejikita katika kutoa sifa za wahusika kwa kurejelea jinsi nne. Haya ni pamoja na: Nafasi ya wahusika, usemi wao, umakundi wa wahusika na ulinganuzi wa wahusika. Sura ya nne nayo imeshughulikia ploti ya kazi hizi. Tumeangazia migogoro, vikwazo, taharuki na vijiploti vilivyokuzwa na waandishi wa kazi hizi ili kujenga msuko wa kazi zao. Sura ya tano inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti na mapendekezo ya tafiti za baadaye.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleFani katika tamthilia ya Kiswahili: Uchanganuzi wa Kilio cha haki na Kijaba cha Moyoen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record