Show simple item record

dc.contributor.authorMutswenje, Sebastian
dc.date.accessioned2013-02-26T08:00:36Z
dc.date.available2013-02-26T08:00:36Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/11542
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia nafasi ya Tamthilia za kihistoria katika Fasihi ya Kiswahili hasa Kinjetekile na Mzalendo Kimathi. Katika sura ya kvvanza kima somo la utafiti, madhumuni, Nadharia Tete, sababu za kuichagua mada hii, yaliyoandikwa kuhusu mada,msingi wa kinadharia pamoja na njia za utafiti.Sura hii kwa hakika ni kama msingi wa kazi hii ya utafiti tulioufanya. Katika sura ya pili tulishughulikia kwa kifupi, dhima ya fasihi kwa jumla, uanishaji wa tamthilia pamoja na ufafanuzi wa tamthilia za kihistoria katika Fasihi ya Kiswahili. Katika kuligusia swala la dhima ya Fasihi tunajiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kubainisha iwapo tamthilia za Kiswahili ambazo ndizo msingi wa utafiti wetu kweli zinatimiza dhima hiyo. Katika sura ii hii uainishaji wa tamthilia unasaidia kuonyesha kwamba tamtiiilia za kihistoria hazipatikani katika ombwe tupu bali ni sehemu ndogo tu ya jamii pana inayobeba aina tofauti tofauti za tamthilia. Sura ya tatu imeshughulikia maudhui katika tamthilia hizo teule za kihistoria. Hayo ni muhimu kwa sababu mojawapo ya malengo ya kimsingi ya Fasihi ni kuelimisha binadamu kupitia mafunzo mbali mbali yanayomwelekeza, kumhamasisha, kumkosoa, kumtahadliarisha na hata kumwonya.Maudhui ndiyo hutoa mchango huu mkubwa katika fasihi. Katika sura ya nne, tumechunguza fani hususan matumizi ya lugha pamoja na wahusika. Kimsingi lugha ndiyo mali ghafi inayotumiwa na binadamu katika sanaa ya fasihi. Kwa hivyo, sehemu hii manuia kuangazia usanii wa lugha ambao unajitokeza katika tamthilia hizi. Kuhusu wahusika tunasema kwamba hao n~iq binadamu wa fasihi wanaotumia lugha hiyo. Vitendo vyao pamoja na tabia zao hupiwa kutokana na aina ya lugha wanaoitumia pamoja na usanii unaojitokeza katika lugha yenyewe. Katika sura ya tano, tumeihitimisha kazi yetu kwa kuonyesha ufanisi wetu hasa kutokana na yale tuliyoyagundua kwa mujibu wa madliumuni pamoja na nadharia tete zetu.Mbali na hayo tmneangazia baadhi ya matatizo yaliyotukumba wakati wa kufanya utafiti wenyewe. Vilevile tulishughulikia mapendekezo kuhusu utafiti fuatilizi unaoweza kufanywa kutokana na mada kama hii.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleNafasi ya tamthilia za kihistoria katika fasihi ya Kiswahili, Kinjeketile (E.Hussein) na Mzalendo Kimathi (Ngugi Na Mugo)en_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record