Upole Na Utoupole Katika Pendo La Karaha
dc.contributor.author | Muteti, Agnes M | |
dc.date.accessioned | 2021-01-19T08:37:17Z | |
dc.date.available | 2021-01-19T08:37:17Z | |
dc.date.issued | 2020 | |
dc.identifier.uri | http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/153653 | |
dc.description.abstract | Utafiti huu unashughulikia upole na utoupole katika Pendo la Karaha. Riwaya hii iliteuliwa kimakusudi ili kupata data iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya kimsingi ya utafiti ilitokana na uchanganuzi wa kauli mbalimbali za wahusika. Kauli za wahusika zilichanganuliwa katika misingi ya nadharia mbili za kipragmatiki. Kila nadharia ilikuwa na wajibu wake tofauti katika kazi hii. Nadharia ya Upole iliyopendekezwa na Brown na Levinson (1987) ilikuwa na wajibu wa kuchunguza upole katika riwaya yote. Nadharia ya Utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) nayo ilitekeleza wajibu wa kuchunguza kuwepo kwa utoupole katika Pendo la Karaha. Lengo la kwanza la utafiti huu lilihusu kuchunguza upole katika riwaya teule. Ilibainika kuwa mikakati ya upole iliyopendekezwa na Brown na Levinson ilidhihirika kikamilifu katika riwaya teule. Lengo la pili la utafiti huu lilikuwa kubaini utoupole katika Pendo la Karaha. Ilibainika kuwa mikakati ya utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) ilidhihirika kikamilifu katika riwaya teule. Lengo la tatu lililohusu kubainisha matendo yanayoathiri nyuso za wahusika liliafikiwa vilevile. Ilibainika kuwa matendo yaliyoathiri zaidi nyuso hasi za wasikilizaji katika Pendo la Karaha yalijumuisha matendo ya msikilizaji kuarifu kuhusu vitendo hasi vijavyo, matendo ya msemaji yaliyoarifu msikilizaji kitendo kilichotarajiwa kuwepo na matendo yaliyoarifu matamanio ya msemaji kwa msikilizaji. Matendo yaliyoathiri nyuso chanya za wasikilizaji yalibainika kupitia matendo yaliyodhihirisha maoni hasi ya msemaji kuhusu uso chanya wa msikilizaji na msemaji kumpuuza msikilizaji | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Nairobi | en_US |
dc.rights | Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States | * |
dc.rights.uri | http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ | * |
dc.title | Upole Na Utoupole Katika Pendo La Karaha | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |