dc.description.abstract | Katika utafiti huu, tumeshughulikia dhima ya tashibihi, sitiari, tashtiti na maelezo ya mandhari katika Utendi wa Ngamia na Paa. Utenzi huu ni miongoni mwa tenzi sita za Kiswahili za jadi zilizokusanywa, kuhaririwa na kutafsiriwa katika lugha ya Kiingereza na J. W. T Allen. Utenzi huu unahusu hadithi ya Ngamia na Paa na jinsi wanyama hawa wawili walitambua nafasi ya Mtume Muhammad katika kukomboa nafsi zao. Katika utafiti huu tumejikita katika kubainisha mchango wa tashibihi, sitiari, maelezo ya mandhari na tashtiti katika ujenzi wa taswira katika Utendi wa Ngamia na Paa. Pia tumechunguza iwapo taswira zinadhihirika wazi wazi kutokana na matumizi ya tashibihi, sitiari, tashtiti na maelezo ya mandhari. Isitoshe, tumechunguza iwapo mtunzi anapotumia mbinu hizi nne katika kazi ya kifasihi ataweza kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe. Tumetumia nadharia ya mtindo ili kupata mwelekeo wa utafiti wetu. | en_US |