Show simple item record

dc.contributor.authorMutuku, Perlice N
dc.date.accessioned2021-08-20T07:57:19Z
dc.date.available2021-08-20T07:57:19Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155292
dc.description.abstractLengo la utafiti huu limekuwa kuchanganua ubanifu wa fani katika hadithi fupi katika diwani ya Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine (2011) iliyohaririwa na Iribemwangi. Mada imechaguliwa kwa misingi kuwa kazi ya kifasihi huzua maana kamili inapochunguzwa kimuundo na kifani. Aidha hadithi fupi zilizoteuliwa hazijawai kufanyiwa uhakiki wa kifani kwa mtazamo wa nadharia ya elimu mitindo. Utafiti wetu umelenga kuchunguza ubanifu katika usawiri wa wahusika na kubainisha nafasi ya matumizi ya lugha katika diwani husika. Nadharia ya elimu- mitindo imetumika katika uchanganuzi wa usawiri wa wahusika na uchambuzi wa kimtindo na imefaa utafiti huu kwa kutoa picha inayodhihirisha baadhi ya sifa za hadithi fupi za kimtindo na kifani kama zinavyodhihirika katika diwani ya Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine. Madhumuni yanayorejelewa yametumiwa kuunda maswali ya utafiti ambayo yametuongoza katika uchanganuzi wa usawiri wa wahusika na uchambuzi wa kimtindo katika diwani hii. Matumizi ya lugha katika diwani husika yamegunduliwa kusheheni methali, semi, tamathali za usemi, sentensi fupi, sentensi ndefu, dayolojia na monolojia. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa matumizi ya lugha yamechangia dhamani ya kiujumi katika hadithi mahsusi na pia kuonyesha namna uhuru wa kutumia lugha katika uandishi huacha athari fulani iliyonuiwa. Utafiti huu pia ulidhihirisha kuwa wahusika katika diwani hii ni wahusika wa mraba mmoja.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisheruniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUbanifu Wa Fanien_US
dc.titleUbanifu Wa Fani Katika Diwani Ya Alidhani Kapata Na Hadithi Nyingineen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States