dc.description.abstract | Tasnifu hii inahusu usawiri chanya wa wahusika wanawake katika tamthilia za Zilizala
na Chamchela. Sura ya Kwanza, mambo muhimu yaliyojadiliwa ni; Utangulizi, Tatizo
la Utafiti, Madhumuni ya utafiti, Nadharia Tete, sababu za kuchagua mada, Upeo na
mipaka ya tasnifu, Msingi wa nadharia na yaliyoandikwa kuhusu mada.
Sura ya pili imeangazia misingi tofauti ya usawiri hasi ambao umekuweko kurnhusu
mwanamke. Misingi hii ni pamojana Fasihi Simulizi, Tenzi, Riwaya, Tamthilia, Hadithi
fupi na Jamii sasa.
Katika Sura ya tatu, usawiri chanya wa rnhusika mwanawake umejadiliwa kwa mujibu
wa tamthilia zilizochaguliwa. Aidha, sababu za waandishi kuwapa wanawake usawiri
chanya pamoja na mchango wa wanawake kwa usawiri wao chanya ni mambo mengine
muhimu yaliojadiliwa.
Mchango hasi na chanya wa wahusika wanaume kwa usawiri chanya wa wanawake
umejadiliwa kwenye sura ya nne.
Sura ya tano ni hitimisho pamoja na mapendekezo kuhusu tafiti za baadaye. Kwa
ujumla, matokeo ya utafiti yametolewa katika sura hii. | en_US |