dc.description.abstract | Utafiti huu unashughulikia arki za simulizi bunilizi katika Utendi wa Mikidadi na
Mayasa. Arki ni sifa za usimulizi wa hadithi bunilizi au halisi. Ni vipengele vya
kimuundo ambavyo hutumika kwa njia tofauti tofauti kulingana na usimulizi husika.
Aidha, ni e1ementi zinazotumika katika usimulizi wa hadithi ili kufanikisha mawasiliano
na uelewa wa hadithi husika. Katika utafiti huu tunatumia nadharia ya naratolojia
mwegemeo wa Rimmon-Kenan (2002). Tunataka kuchunguza na kuthibitisha kuwa kuna
matumizi ya usimulizi katika ushairi kama ilivyo katika riwaya.
Tunaigawanya kazi yetu katika sura sita. Katika sura ya kwanza tunajadili somo la utafiti,
madhumuni ya utafiti, maswali ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka,
misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mad a na mbinu za utafiti.
Katika sura ya pili tunashughulikia usimulizi, usimulizi wa hadithi, sampuli za
wasimulizi, viwango vya usimulizi, uhusika wa msimulizi hadithini, uhusika na mhusika,
wakati wa usimulizi, utegemefu wa msimulizi na hadhi ya msimulizi.
Katika sura ya tatu nayo tunachunguza mpangilio wa matukio katika hadithi ambao
umegawanywa katika mikondo mitatu: mpangilio wa matukio katika mfuatano wa
wakati, muda katika usimulizi na idadimarudio ya matukio katika hadithi.
vii
Tunahakiki mtazamo katika sura ya nne ambao unachukua sura mbalimbali kama vile
sura ya mwanda wakati na mwanda mahali, sura ya saikolojia na sura ya itikadi.
Katika sura ya tano tunashughulikia uwasilishaji wa usemi na mawazo. Tunatalii usemi
halisi na mawazo halisi, usemi halisi huru na mawazo halisi huru, usemi taarifa na
mawazo taarifa na usemi taarifa huru na mawazo huru. Sura ya sita ni hitimisho la kazi
nzima, matokeo ya utafiti na mapendekezo kuhusu tafiti za baadaye. | en_US |