Show simple item record

dc.contributor.authorLikhako, Pamela I
dc.date.accessioned2021-09-08T05:41:53Z
dc.date.available2021-09-08T05:41:53Z
dc.date.issued1991
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155445
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza ufaaji wa Kiswahili kama lugha ya k' _unzia katika viwango vyote vya elimu. Tumechunguza ~shelezaji wa Kiswahili katika kufunza hasa masomo ya Kisayansi na t- ~uma za kiufundl Tumezingatia hasa Istilahi zilizoko katika masomo ya sayansi na ya kiufundi katika viwango vyote vya elimu na utoshelezaji wa hizi istilahi. Tasnifu hii imeonyesha kwamba Kiswahili kinatosheleza na kinafaa kama lugha ya kisomo. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni dibaji inayotanguliza kazi hii. Katika sura hii tumeeleza mada ya somo letu la utafiti na madhumuni ya tasnifu hiyo. Ni katika sura hii ambapo tunazijadili sababu za kuchagua somo hili, mipaka ya tasnifu hii na msingi wa nadharia tuliyoiegemea katika utafiti wetu. Aidha tumejadili kazi za watu mbali mbali waliochunguza kazi inayohusiana na yetu na tukadokeza na haipothesia zetu. Tumeihitimisha kazi hii kwa kuzieleza njia tulizozitumia katika utafiti huu. Katika sura ya pili, tumejadili hali ya lugha nchini Kenya. Tumejaribu kujadili sababu zinazofanya hali ya lugha kuwa ilivyo. Tumeangalia mfumo wa elimu ya 8.4.4 na athari zake hasa kwa lugha ya Kiswahili. Ni katika sura hii ambapo tumejadili lugha ya sayansi na pia kuchunguza sababu za kudhania kwamba Kiswahili chafaa kama lugha ya kisomo. Katika sura ya tatu tumegusia mashirika na watu mbalimbali wanaoshughulikia uundaji wa istilahi. Pia tumezungumzia njia zinazotumika kuundia istilahi na tukachunguza ubora na udhaifu wa kila njia. Katika sura ya Nne tulijish~ghulisha na kuchunguza istilahi zilizopo katika masomo tuliyoyachagua ya Kisayansi na ufundi katika viwango mbalimbali vya elimu yaani katika elimu ya msingi, elimu ya upili na elimu ya vyuo. Sura ya tano ni hitimisho pamoja na kuchunguza matatizo yanayokikumba Kiswahili nchini Kenya~en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUfaaji Wa Kiswahili Kama Lugha Ya Kisomoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States