Show simple item record

dc.contributor.authorSabula, Millicent A
dc.date.accessioned2021-09-08T05:51:00Z
dc.date.available2021-09-08T05:51:00Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155446
dc.description.abstractFasihi ya kiekolojia ru uwanja uliochipuka miaka ya 1970 na kuendelea rniaka ya 1990 kuchanganua, kuchambua na kuhakiki kazi za kifasihi. Uwanja huu unalenga kuangazia fani na maudhui katika matawi ya fasihi kiekolojia kama vile ya Kiafrika, Kimarekani na Kiferninisti. Utafiti huu unahusu nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira kwa mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojia. Lengo kuu la utafiti huu ni kupambanua mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni haya: kubainisha mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto; kupambanua mhusika Nakuruto na mchango anaoutoa katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira; kujadili kwa kina changamoto anazopitia mwanawake katika kuhifadhi mazingira; kujadili athari za masuala ya kirnazingira na jinsi zinavyojitokeza katika riwaya. adharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa kiekolojia iliyoasisiwa na mfaransa Francoise d'Eaubonne mwaka wa 1974. Nadharia hii ilibuniwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya kiekolojia hasa kwa kumzingatia mwanarnke. Utafiti huu ulifuata muundo wa uchanganuzi wa makala ambapo maelezo yetu yaliangazia masuala tata yaliyoko kwenye matini tuele. Maka1a ya kimsingi ya utafiti yalikuwa ni riwaya ya Nakuruto ilhali rnakala ya sekondari yalitokana na usomaji wa vitabu na makala yaliyohusu mada. Utafiti huu ulibainisha kwamba uferninisti wa kiekolojia una nafasi ya kuwazindua wanawake ili kuleta ukornbozi wa kimazingira. Aidha, utafiti ulitambua kuwa mhusika Nakuruto aliwazindua wanajarniikupitia kwa el imu na maarifa yake ya kimazingira, hivyo kusababisha mapinduzi. Utafiti ulitambua kwamba wanawake wanasimangwa, kutukanwa, kudharauliwa na kudunishwa wanapojihusisha na harakati za utunzaji mazingira. Mwisho utafiti ulitarnbua kwarnba umaskini, kukauka kwa chernichemi za maji, uskwota, magonjwa na vifo ni athari zinazosababishwa na uharibu wa mazingira. Utafiti huu ulihitimisha kwarnba mwanamke anastahili kupewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira na kwamba, fasihi ya Kiswahili ina uwezo wa kumulika masuala ya kielokojia kama yanavyojitokeza katikajamii. Kwa kuwa utafiti huu haukuweza kuchunguza vipcngele vyote vya kifasihi mazingira, mtafiti anapendekeza kwamba utafiti wa baadaye uzingatie mikabala minginc kama vile fasihi mazingira kieneo, Kiafrika na Kimagharibi, hasa kwa mkondo wa kilinganishi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleNafasi Ya Wanawai Katika Uhifadhi Wa Mazinglra Katika Riwaya Ya Nakuruto- Mtazamo Wa Fasihi Ya Ufeministi Wa Kiekolojiaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States