dc.description.abstract | Utafiti huu umehusu maudhui na mtindo katika Utenzi wa Vita vya Uhud wa Haji
Chum (1959). Tumechunguza maudhui mbalimbali yanayojitokeza kwenye utenzi
huu. Tumeshughulikia vipengele mbalimbali vya kimtindo vikiwemo wahusika,
dayolojia, tamathali za serru na kunga nymginezo. Tamathali za serm
tulizozishughulikia ni pamoja na sitiari, tashbihi, chuku, uhuishaji, maswali ya
balagha na tabaini. Kunga nyingine tulizozishughulikia ni urudiaji, takriri, misemo na
ukiushi wa kisintaksia. Tumeongozwa na nadharia mbili: nadharia ya Umuundo na ile
ya Uhalisia. Tumeongozwa na malengo matatu ya utafiti: kwanza, tumechunguza
maudhui yanayojitokeza kwenye utenzi, pili, tumeeleza jinsi wahusika
wanavyoendeleza maudhui hayo na tatu, tumechunguza jinsi baadhi ya vipengele
vingine vya kimtindo vinavyoendeleza maudhui. Tumebaini kuwa maudhui ya dini,
ushujaa, vita na mauaji yamejitokeza katika utenzi. Pia, mtunzi amefanikiwa
kuwatumia wahusika kuendeleza maudhui haya na mwisho, mbinu nyinginezo za
kimtindo alizotumia mtunzi ni pamoja na taswira, dayolojia na tamathali za usemi
ambazo kwa pamoja zimefanikisha kuchimuza maudhui. Hatimaye, tumetoa
mapendekezo ya tafiti za baadaye. | en_US |