Show simple item record

dc.contributor.authorMatundura, Enock S
dc.date.accessioned2021-09-09T05:33:48Z
dc.date.available2021-09-09T05:33:48Z
dc.date.issued2007
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155454
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu limekuwa ni kubainisha Jll1Sl taswira durnifu za uana zinavyojitokeza katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Nadharia tete tatu zilizoongoza utafiti huu ni: Mosi, taswira dumifu za uana zinadhihirika katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Pili, wahusika katika fasihi ya Kiswahili ya watoto husawiriwa kwa njia sawa bila kubaguliwa kwa misingi ya jinsia zao. Mwisho, waandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili ya watoto huwakilisha idadi sawa ya wahusika wa kike na kiume katika kazi hizo. Kupitia kwa utafiti huu, nadharia tete ya kwanza imethibitishwa kuwa kweli. Lakini nadharia tete ya pili na ya tatu zimethibitishwa kuwa si kweli. Mikabala ya uana na ufeministi ambayo imetumika katika utafiti huu ilitoa msingi madhubuti katika utafiti huu ila tulilazimika kuitumia kwa tahadhari kwa sababu inaakisi rnno tamaduni za Kimagharibi. Kuna juhudi zinazofanywa za kutafuta mkabala wa ufeministi unaoafiki zaidi uhakiki wa fasihi ya Kiafrika. Tasnifu hii ina sura tano zinazoshughulikia kipengele cha taswira dumifu za uana katika fasihi ya Kiswahili ya watoto ifuatavyo: Sura ya kwanza inatoa kwa ujumla mwelekeo wa kuchunguza jinsi taswira dumifu za uana zinavyoweza kudhihirishwa katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Inahusisha sehemu kuhusu somo la utafiti, malengo, nadharia tete, sababu za kuchagua somo hili, yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka na njia za utafiti. Sura ya pili irnejadili kwa ujumla kuhusu Iasihi ya watoto, sifa na majukumu yake. tofauti kati ya dhana 'uana' najinsia. Aidha sura hii irnezungumzia taswira dumifu. Katika sura za tatu na nne, tumechunguza matini za tungo za fasihi ya Kiswahili ya watoto za waandishi wa kiume (androtexts) na kike (gynotexts) mtawalia ili kubainisha jinsi taswira dumifu za uana zinavyojitokeza. Kadhalika katika sura hizi, tumechunguza iwapo wahusika wa kike na kiume wamewakilishwa kwa idadi sawa kwenye matini hizo. Sura ya tano ni hitimisho. Ina sehemu za muhtasari wa matokeo ya utafiti huu kwa misingi ya nadharia tete zilizoongoza uchunguzi huu, matatizo tuliyokumbana nayo katika utafiti huu na mapendekezo kuhusu utafiti zaidi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleTaswira Dumifu Za Uana Katika Fasihi Ya Kiswahili Ya Watotoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States