Show simple item record

dc.contributor.authorMutua, John M
dc.date.accessioned2021-09-09T05:52:59Z
dc.date.available2021-09-09T05:52:59Z
dc.date.issued2007
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155456
dc.description.abstractMadhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kushughulikia swala la mitazamo ya vijana na wazee kuhusu ukombozi wa mwanamke katika tamthilia tatu za Kiswahili. Tamthilia zilizoteuliwa ni: Kitumbua kimeingia mchanga (2000) S. Mohamed, Migogoro (2006) M. Mbatiah na Natala (1997) K. wa Mberia. Pamoja na kazi hizi pia tulipitia kazi mbalimbali zilizohusiana na mada ya utafiti ili kujifahamisha na maswala yanayohusu wanawake. Sura ya kwanza ni usuli wa utafiti ambapo somo la utafiti, madhumuni, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zimeshughulikiwa. Aidha, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo hili pamoja na njia za utafiti zimeangazi wa. Sura ya pili inachunguza namna mbalimbali ambavyo wanawake wanadhulumiwa kwa mujibu wa kazi hizi tatu. Vile vile, tumejadili baadhi ya juhudi zinazofanywa ili kumkomboa mwanamke. Pamoja na hayo, tunamulika baadhi ya changamoto zinazozikabili harakati za kumkomboa mwanamke. Katika sura ya tatu tunajihusisha na mitazamo ya vijana wa kike na wa kiume kuhusu ukombozi wa mwanamke. Aidha, tunachunguza baadhi ya sababu zinazowapelekea vijana kuwa na mitazamo hiyo. Sura ya nne inashughulikia mitazamo ya wazee wa kike na wa kiume kuhusu swala la ukombozi wa mwanamke. Vile vile, sababu za wazee kuwa na mitazamo hiyo zinachunguzwa. Mwisho, tunalinganisha mitazamo ya vijana na wazee. Katika sura ya tano tunatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo kuhusu tafiti za baadaye.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMitazamo Ya Vijana Na Wazee Kuhusu Ukombozi Wa Mwanamke Katika Tamthilia Tatu Za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States