Show simple item record

dc.contributor.authorMoraa, Lydiah
dc.date.accessioned2021-09-09T06:39:44Z
dc.date.available2021-09-09T06:39:44Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155459
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu uchanganuzi wa matatizo katika matini tafsiri za kimatibabu kutoka lugha ya Kiiingereza hadi Kiswahili. Umuhimu wa mawasiliano katika taaluma ya kimatibabu ni jambo ambalo haiwezi kufumbiwa macho kwa kuwa hitilafu huweza kuathiri maisha. Mara nying: watafiti wa taaluma ya tafsiri wameshughulikia matatizo katika fasihi na katika vitabu vya kidini. Urafiti huu umelitoa swala la tafsiri nje ya mipaka ya iliyozoeleka kwa kutolea mchango wa kiusomi na kiutekelezi katika taaluma ya kimatibabu. Tumeainisha matatizo ya kiisimu na yasiyo ya kiisirnu. Tumefanya hivyo kwa kutambua matatizo katika matini za kimatibabu na kupcndekeza mikakati za kukabiliana nayo. Mawasilliano baina ya rnhudumu wa afya kama vile madakiari na wahudumumiwa hukumbwa na mapengo kwa sababu ya tofauti ya ujuzi wa lugha ya kimatibabu na tofauti za miundo baina ya lugha ya Kiingereza na Kiswahili kuhusu uhalisi wa aina mbalimbali. Kwa matumizi ya nadharia ya Hearvy na Higgins (1992) tunatarnbua pcngo 1<1 kirnawasiliano baina ya madaktari na wateja wao wasio na ujuzi wa msamiati wa k irnatibabu. Huu ni utafiti kielelezo katika hospitali ya Kisii Level 5 Katika sura ya kwanza, tumeangazia mada hii kwa kuanzia: utangulizi, tatizo la utafiti. rnadhumuni, sababu za kuchagua somo, mipaka na upeo, yaliyoandikwa, misingi ya nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili imeangazia dhana mbalimbali katika tafsiri nazo ni: dhana ya tafsiri. aina za tafsiri, maana katika tafsiri na mawasiliano katika tafsiri. Pia tumeangazia uhusiano baina ya tafsiri na taaluma nyingine kama vile: fonolojia, mofolojia, sintaksia. scmantiki. pragmatiki.saikolojia na utarnaduni. Sura ya tatu ndiyo kiini cha tafsiri yetu arnbapo tumeangazia matatizo halisi ya m.uini ZCl kirnatibabu kwa njia ya kiulinganishi kwa kutumia data ya Kiingereza na ya Kiswahili. Turncgawa matatizo katika makundi mawili; ya kiisimu ya yasiyo ya kiisimu. Hatimaye katika sura ya nne, tumetoa matokeo ya utafiti na kutoa mapendekezo yetu. Mbali na hayo tumetoa mchango wetu wa kiutekelezi kwa kupendekeza njia za kukabiliana na matatizo yanayojitokeza. Pia turnependekeza tafsiri kwa baadhi ya msamiati uliokosa kutafsiriwa.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMatatizo Yanayodhihirika Katika Matinl Tafsiri Za Kimatibabu Kutoka Kiingereza Hadl Kiswahili: Utafiti Kielelezo Katlka Hospitali Ya Kisii Level 5en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States