dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia taswira ya mwanamke katika tamthilia mbili za Kiswahili.
Tumeangalia picha ambayo mwanamke amepewa na jamii katika tamthilia za Kilio
Cha Haki (1981) na Pango(2003).
Katika sura ya kwanza tumeshughulikia tatizo la utafiti,madhumuni ya utafit,nadharia
tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, yal iyoandikwa juu
ya mada na njia za utafiti.
Katika sura ya pili tumeshughulikia taswira hasi na chanya aliyopewa mwanamke na
jamii katika tamthilia ya Kilio cha Haki (1981) Alamin Mazrui na kisha tukaangazia
njia ambazo mwanamke anaweza kuzitumia ili kujikomboa.
Sura ya tatu imeshughulikia taswira chanya na hasi aliyopewa mwanamke na jamu
katika tamthilia ya Pango (2003) Wamitila K.W na vilevile tukaonyesha njia ambazo
mwanamke anaweza kutumia ili kujikomboa.
Sura ya nne imeshughulikia hitimisho la utafiti wetu pamoja na mapendekezo. | en_US |