dc.description.abstract | Tasnifu hii imechunguza namna taswira ya gereza inavyotumiwa kuendeleza maudhui
katika Haini riwaya ya Adam Shafi. Tasnifu hii ina sura tano.
Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia
tete, sababu za kuchagua somo, msingi wa nadharia, upeo na mipaka, yaliyoandikwa
kuhusu sorno na vilevile njia tulizozitumia katika utafiti huu.
Katika sura ya pili, tumefafanua dhana muhimu tunazitumia katika utafiti huu.
Tumezifafanua dhana za taswira, maudhui, gereza na jamii ya kigereza. Ufafanuzi wa
dhana hizi urnekuwa muhimu kwa kuwa umeweka rnisingi ya kukusanya na kuchanganua
data ya utafiti wetu.
Sura ya tatu imeangazia namna sifa za jamii ya kigereza zinavyojitokeza katika Haini.
Kwa hivyo, katika sura hii tumefafanua namna maudhui ya jamii ya kigereza
yanavyosawiriwa na kuendelezwa riwayani.
Baada ya kuonyesha namna sifa zajamii ya kigereza zinavyojitokeza riwayani, sura ya nne
irneonyesha athari za jamii ya Kigereza kwa mujibu wa riwaya ya Haini.
Sura ya tano ni hitimisho la utafiti wetu. Katika sura hii, pia tumetoa mapendekezo ya
utafiti zaidi kuhusu riwaya hii ya Haini. | en_US |