dc.description.abstract | Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kushughulikia swala la mitazamo ya vijana na
wazee kuhusu ukombozi wa mwanamke katika tamthilia tatu za Kiswahili. Tamthilia
zilizoteuliwa ni: Kitumbua kimeingia mchanga (2000) S. Mohamed, Migogoro (2006)
M. Mbatiah na Natala (1997) K. wa Mberia. Pamoja na kazi hizi pia tulipitia kazi
mbalimbali zilizohusiana na mada ya utafiti ili kujifahamisha na maswala yanayohusu
wanawake.
Sura ya kwanza ni usuli wa utafiti ambapo somo la utafiti, madhumuni, sababu za
kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zimeshughulikiwa.
Aidha, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo hili pamoja na njia za utafiti
zimeangazi wa.
Sura ya pili inachunguza namna mbalimbali ambavyo wanawake wanadhulumiwa kwa
mujibu wa kazi hizi tatu. Vile vile, turnejadili baadhi ya juhudi zinazofanywa ili
kumkomboa mwanamke. Pamoja na hayo, tunamulika baadhi ya changamoto
zinazozikabili harakati za kumkomboa mwanamke.
Katika sura ya tatu tunajihusisha na mitazamo ya vijana wa kike na wa kiume kuhusu
ukombozi wa mwanamke. Aidha, tunachunguza baadhi ya sababu zinazowapelekea
vijana kuwa na mitazamo hiyo.
Sura ya nne inashughulikia mitazamo ya wazee wa kike na wa kiume kuhusu swala la
ukombozi wa mwanamke. Vile vile, sababu za wazee kuwa na mitazamo hiyo
zinachunguzwa. Mwisho, tunalinganisha mitazamo ya vijana na wazee.
Katika sura ya tano tunatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo
kuhusu tafiti za baadaye. | en_US |