Show simple item record

dc.contributor.authorNdung'u, Mary N
dc.date.accessioned2021-09-13T09:26:42Z
dc.date.available2021-09-13T09:26:42Z
dc.date.issued2009
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155466
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Tumechunguza na kuchanganua tungo ambazo hutambulisha mada na fokasi huku tukitolea maelezo na ufafanuzi wa kina, Malengo ya utafiti huu ni kuchunguza ikiwa kuna uhusiano kati ya mada na fokasi. Pia tumechunguza utambulishaji wa mada na fokasi huku tukitathmini ikiwa mada na fokasi huweza kutambulishwa kwenye kirai. kishazi au kileksika. Mwisho tumetathmini kufanikiwa kwa Mtazamo wa Muundo wa Taarifa katika utarnbulishaj i wa mada na Iokasi katika Kiswahili Sanilu. Nadharia ambayo imetuongoza katika utafiti huu ni Mtazamo wa Muundo wa Taarifa iliyoasisiwa na Wanaisimu wa Shule ya Prague, ikaendelezwa na Halliday (1967) na baadaye kukuzwa zaidi na Lambrecht (1994), Muundo wa taarifa husimbwa katika sentensi katika utambulishaji wa mada na fokasi ili kubainisha ni sehernu gani ya seniensi inayobeba taarifa mpya na ni sehemu gani inayobeba taarila inayojulikana. Katika uchanganuzi wa data. tumeteua data kutoka riwaya ya f\1I1i ya Adam Shafi (1979) ambayo tumetumia kama data ya kimsingi. Aidha tumepata data zaidi kutoka makala mbalimbali zilizochapishwa. Zaidi ya hayo tumezalisha data ili kukidhi mahitaji yetu katika uchanganuzi wa tungo ambazo hutarnbulisha mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti huu. lmejumlisha utangulizi. mada ya utafiti. madhumuni ya utafiti. nadharia tete. sababu za kuchagua mada hii. upeo na mipaka. uhalalishaji. msingi wa kinadharia. yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia maswala ya kimsingi yanayohusiana na mada, fokasi na msingi wa kinadharia wa Muundo wa Taarifa. Katika sura ya tatu. tumeshughulikia na kuchanganua tungo ambazo hutambulisha mada. Tumepata kuwa mada katika sentensi huhitaji kuakisiwa kama vile katika kuitanguliza katika sentensi. kuihamislia kushoto . . . . . . rruongoru mwa njia zingme. Sura ya nne imejikita katika uchanganuzi wa clata katika tungo ambazo hutambulisha fokasi katika Kiswahili Sanifu. Tumechunguza aina za Iokasi kama vile fokasi kwenye kiarifu, Iokasi kwenye KN na fokasi katika senteusi miongoni mwa aina zingine za Iokasi. Katika sura ya tano. tumeangalia jinsi mada na fokasi huhusiana katika muktadha wa utambuzi. uchochezi. na ulinganuzi. Tumepata kuwa mpangilio wa rnaneno katika sentensi huwa na mchango mkubwa katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu arnbao huwa huru kwa kiasi. Sura ya sita inabeba hitimisho na mapendekezo ya utafiti huu. Katika hitimisho tumetoa matokeo ya utafiti yanayohusiana na utambulishaji wa mada na Iokasi katika Kiswahili Sanifu. Mapendekezo ambayo tumetoa yatachochea tafiti zaidi katika uwanja huu. Tumependekeza kuwa tafiti zaidi zifanywe katika uchanganuzi wa data \\\:1 kimofosintaksia katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Pia tafiti zaidi ambazo zitaongozwa na nadharia tofauti au utafiti katika usimbaji wa rnuundo wa taarifa kwenye tungo changamani za kimofosintaksia au za kiarudhien_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMada Na Fokasi Katika Kiswahili Sanifu: Mtazamo Wa Muundo Wa Taarifa.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States