dc.description.abstract | Katika utafiti huu wa ukombozi wa mwanamke, tumeona kwamba ukombozi wa
mwanamke unamtegemea mwanamke mwenyewe. Mwanamke anafaa kuchukua mstari
wa mbele ili kupigania haki zake za kijamii kama njia ya kupinga ugandamizwaji
anaotendewa na mwanamume. Ili kutimiza haya inafaa mwanamke ajikomboe katika hali
zote za maisha kama vile: kijamii, kiuchumi na kisiasa. Anapofikia hali hii, mwanamke
ataweze kujitegemea katika utendakazi na kuchukua uamuzi wa busara katika jamii.
Kufanya hivi kutaweza kumwondolea majaribio yanayolenga kumgandamiza.
Katika utafiti huu tumeweza kuonyesha namna wahusika wa kike katika riwaya za
Habwe wamejishughulisha na harakati mbalimbali zinazolenga kuwakomboa kutokana
na ugandamizaj i wa wanaume.
Katika sura ya pili tumeweza kutaja baadhi ya riwaya zingine za mwandishi ambazo kwa
ujumla zinanuia kuleta heshima, haki, usawa na ushirikiano katika jimii. Aidha tumeweza
kujadili hali mbalimbali za ukombozi wa kijamii, kiuchumi na kisiasa. Tumejadili kuhusu
dhuluma wanazopitia wanawake kutoka kwa wanaume. Baadhi ya dhuluma hizi ni:
kupewa adhabu kali, kulazimishwa katika ridoa, kubaguliwa katika urithi, kubaguliwa
katika taasisi za elimu na kubaguliwa katika uongozi. Ugandamizaji huu hutekelezwa na
vyombo vya kijamii kama vile: Utamaduni ndoa na dini.
Katika sura ya tatu na ya nne tumejadili kuhusu harakati za kujikomboa dhidi ya dhuluma
za mwanaume. Kupitia riwaya ya Maumble sf Huja. Tumeonyesha naruna mwanamke
amejiimarisha kiuchumi na kijamii lakini kwa kiasi kikubwa kwa kutegemea nguvu za
vi
mwanamume. Riwaya hii imeonyesha mwanzo tu wa harakati za ukombozi ambapo
mwanamke amejikomboa kwa kiasi kidogo.
Kwa kutumia mali ya mwanamume, mwanamke amejianzishia miradi ambayo
imefanikiwa japo kwa kiasi kidogo. Riwaya ya Fumbo la Maisha, mwanarnke ameweza
kujikomboa kiuchumi, kijamii na kisiasa. Amedhihirisha hayo wazi kwa kuanzisha
miradi yake ya kiuchumi kama vile biashara, kilimo, na ufugaji. Hatimaye amefikia upeo
wa kudai na kupewa haki zake kama vile ardhi haki ya kuiongoza jamii kwa
kuchaguliwa mbunge. | en_US |