dc.description.abstract | Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchanganua dhamira ya uozo katika nwaya ya
Upotevu, kuchunguza uhusika unavyotumiwa kuendeleza uovu na kuonyesha madhara ya
uovu katika jamii.
Kazi hii ina sura tano. Katika sura ya kwanza, tumetoa pendekezo la utafiti linalojumulisha
tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Katika sura hii
pia tulishughulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, msingi wa nadharia,
yaliyoandikwa kuhusu mada na nj ia za utafiti. Tulitumia mbinu ya maktabani katika
kukusanya data tuliyohitaji na kuichanganua.
Katika kazi hii, tulitumia nadharia ya Maadili kwa sababu riwaya hii ya Upotevu ma
maudhui mengi yanayodhihirisha ukiukaji wa maadili katika jamii.
Katika sura ya pili, tulishughulikia dhamira ya uozo katika riwaya ya Upotevu. Waaidha,
sura ya tatu imechunguza namna uhusika ulivyotumiwa kuendeleza uovu. Tumezungumzia
wahusika wa kitaashira wenye matendo merna na maovu.
Katika sura ya nne, tumebainisha madhara ya uozo katika jamii kwa kurejelea kikamilifu
riwaya ya Upotevu.
Sura ya tano ni hitimisho. Katika sura hii tumetoa maoni kuhusu tasnifu hii pamoja na
mapendekezo ya kufanya kwa utafiti zaidi. | en_US |