Show simple item record

dc.contributor.authorMugwika, Ferinda K
dc.date.accessioned2021-09-24T10:08:37Z
dc.date.available2021-09-24T10:08:37Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155516
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu dhana ya uchimuzi katika uendelezaji wa riwaya ya kimajaribio au mpya ya Mafamba (2008). Ni riwaya ya kwanza ya Olali inayomulika hali ya kisiasa katika jamii yetu na harakati za wananchi za kuwang'oa viongozi wadhalimu. Katika kuitafiti kazi hii, tuliongozwa na mwelekeo wa kihakiki wa Urasimu wa Kirusi. Utafiti huu unahusu nafasi ya uchimuzi katika nwaya ya Mafamba. Suala ambalo tumeshughulikia kwa kuangazia uchimuzi katika ngazi ya wahusika na matumizi ya lugha. Utafiti huu ulilenga kudhihirisha kuwa, uchimuzi ni nguzo kuu katika uendelezaj i wa riwaya ya kimajaribio au mpya ya Mafamba. Tumeigawa tasnifu hii katika sura tano. IIi kufikia malengo yetu, sura ya kwanza imeshughulikia utangulizi kwa ujumla. Utangulizi huu unahusu usuli wa mada, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete. sababu za kuchagua mada, mipaka na upeo. misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumezungumzia msuko wa riwaya ya Mafamba ambao unajenga msingi wa uelewa wa riwaya hii. Tumeiona riwaya hii kuwa ya kuvutia na kusisimua hasa kutokana na usimulizi wake unaoelezea masuala nyeti ya kisiasa ya jamii yetu katika mtindo mpya wa uandishi kwa njia inayokiuka sifa za uandishi wa riwaya za jadi. Katika sura ya tatu tumeshughulikia uchimuzi katika kiwango cha wahusika. Uchimuzi huu unatokea katika kiwango cha maana au kisemantiki. Tumebainisha kwamba, uchimuzi wa wahusika katika riwaya ya Mafamba unabainika kupitia kwa usawiri wao kiasi cha kubatilisha dhana nzima ya uhusika hata ingawa matendo yao na wasifu wao unachukuana na hali ya kisasa ya maisha ya jamii yetu kwa jinsi tunapata kuwatambua, kutambua tabia zao na mielekeo yao. xi Aidha kupitia kwa uchimuzi katika kiwango hiki, dhamira ya mwandishi na aidha maudhui katika riwaya hii yanabainika. Sura ya tatu inahusu uchimuzi katika kiwango cha matumizi ya lugha. IIi kufanikisha lengo letu, tuliangazia vipengele vya matumizi ya lugha katika kiwango cha kimsamiati na kisemantiki. Utafiti wetu umebaini kuwa, viwango hivi vinachimuza sifa zilizozungumziwa na Wana- Urasimu kama uajinabishaji au kufanya kazi ya kifasihi kuonekana kuwa ngeni, matumizi ya mbinu kadha za uwasilishaji na matumizi ya kipekee ya lugha. Sura ya tano inahusu hitimisho la utafiti. Katika sehemu hii, tumerejelea mada ya utafiti huu na maswala ya kimsingi tuliyoyaelezea katika sura ya kwanza. Kutokana na matokeo ya uchanganuzi data yetu, tumerejelea nadharia tete zetu ili kuzikubali na pia tumetoa mahitimisho na mapendekezo ya utafiti wa baadaye.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectDhana Ya Uchimuzien_US
dc.titleDhana Ya Uchimuzi Katika Uendelezaji Wa Riwaya Ya Kimajaribio Ya Mafambaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States