dc.description.abstract | Kazi hii Lnahakiki, maudhui ya kiukCi.mbozikatika
tamthilia tatu ambazo ni Mukwawa wa Uhehe, Kinjeketile,
na Mzalendo Kimathi. Tasnifu hii i~iki taswira ya
Mwafrika katika vita vya ukombozi dhidi ya ukoloni
katika Afrika Mashariki. Swala hili limeshughulikiwa
katika viwango viwili. Kwanza taswira ya M~afrika
imechambuliwa katika tamthilia zinazohusika. Kisha
nadharia inayohusu uyakinifu katika kazi za kifasihi
imetumika kuchambulia uyakinifu wa taswira hii.-
Ina sura sita kwa jumla. Sura ya kwanza imeshughulikia
mada ya utafiti, madhumuni, msingi wa kinadharia
wa utafiti, udurusi wa yaliyoandikwa kuhu su mada hii,
sababu za kuchagua mada hii, upeo wa utafiti, na njia
zil~zotumika katika utafiti huu. Ni sura inayoonyesha
mpango wa kazi hii.
Sura ya pili inashughulikia maelezo ya kljumla
kuhusu jukumu la fasihi katika ukombozi pamoja na
msingi wa kihistoria wa fasihi ya kiukombozi katika
Afrika Mashariki. Sura ya tatu inashughulikia tamthilia
ya Mukwava wa Uhehe, ya nne Kinjeketile, na ya tano
Mzalendo Kimathi. Katika kila sura, ni kipengee muhimu
zaidi na kinachojitokeza wazi zaidi katika tamthilia
inayoshughulikiwa ambacho kimesisitizwa.
Kila sura inaishia kwa hitimisho lake. Hili
linatoa muhtasari wa vipengee muhimu~navyojitokeza
kuhu su o-iwa f rLka katika tamthilia inayohusika.
Hatimaye kuna hitimisho jumuishi la mada ~zima.
Hitimisho hili linatoa mapendekezo ya utafiti zaidi
na matatizo tuliyokumbana nayo katika utafiti huu.
Mwisho tumetoa orodhaya marejeleo muhimu kuhusu mada inayoshughulikiwa. | en_US |