dc.description.abstract | Fani ni jumla ya vipengele vya kimtindo au kisanaa vinavyotumiwa kuwasilisha ujumbe.
Katika tenzi vipengele vinavyojitokeza ni mtindo, muundo, toni, msuko, mandhari,
wahusika, wakati, matumizi ya lugha na vipengele vingine vya kisanaa.
Tumeigawanya tasnifu hii katika sura nne. Sura ya kwanza inaeleza dhamira yetu kwa
kufafanua dhana za somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu ya kuchagua somo,
yaliyoandikwa kuhusu somo, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, nadharia tete na njia
za utafiti. Sura ya pili inachanganua dhana ya fasihi simulizi, maana ya ushairi, chimbuko
la ushairi, maendeleo ya ushairi, athari za wageni, mashairi huru na lugha ya ushairi.Sura
ya tatu inafafanua vipengele vya kimtindo, matumizi ya lugha na vipengele vya kisanaa.
Sura ya nne inafananua nadharia tete tano.
Kwa ufupi, nadharia tete ya kwanza inasema kuwa mtunzi ametumia msamiati akilenga
hadhira ya kisasa. Maneno kama keshi (20), saini (204), baiskeli na motukari (277) n.k ni
maneno yanayotuonyesha taathira za msamiati wa Kiingereza. Hawa ndio wageni
waliofika mwisho baada ya Wareno na Waarabu ambao athari zao pia zinapatikana
kwenye msamiati wa watu wa Kilwa. Neno malaya la Kiswahili lina asili ya neno malay
la Kireno, yaani mtumishi wa kike anayetoka nchini Malay. Neno mvinyo la Kiswahili
limetoholewa kutokana na neno vinho la Kireno. Pia neno msabiki (24), akaqimu (42) n.k
ni maneno yaliyotoholewa kutokana na msamiati wa Kiarabu, Kwa hivyo, mvurugo huo
ulioikumba lugha ya ushairi wa Kiswahili unadhihirisha kuwa hadhira hii imeingiliana na
wageni kabla ya, wakati wa na hata baada ya uhuru. Bali hii ya maingiliano
inadhihirishwa kutokana na utohozi wa msamiati wa wageni; hii ina maana kuwa hadhira
hii ni ya kisasa.
Ya pili inasema kwamba baadhi ya wahusika hubadilisha toni kulingana na hadhira.
Anapoongea na wachawi wenzake, Shambi hutusi, hukaripia na huarnrisha. | en_US |