Show simple item record

dc.contributor.authorOnchwati, Jared, S
dc.date.accessioned2021-10-01T12:59:39Z
dc.date.available2021-10-01T12:59:39Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155582
dc.description.abstractUtafiti huu ulikusudia kuonyesha sifa za kiuhalisiajabu kama zinavyojitokeza katika Ukawafi wa Miiraji na Utenzi wa Fumo Liyongo. Tulifanyanya hivyo kwa kuwarejelea baadhi ya wahusika na mandhari kama yalivyosawiriwa katika tcnzi zenyewe. Madhumuni yetu katika utafiti huu yalikuwa kudhihirisha uhalisiajabu ulivyosawiriwa katika tenzi. Aidha tulibaini kuwa sifa za kiuhalisiajabu zilikuwa nguzo muhimu kwa watunzi wa tenzi hizi katika kufikia malengo yao mbali na wao kutengana kiwakati na kiumri. Tuliufikia uchanganuzi huu baada ya kutambua kuwa, uhalisiajabu katika tenzi haujatafitiwa sana ilihali ni mojawapo ya fasihi kongwe zaidi kuliko riwaya na tamthilia. Tumeangalia sifa za takribani wahusika wote katika tenzi hizi, mazingira walimolelewa pamoja na jamii zilizowazaa na kuwalea. Vile vile tumeangalia umuhimu wao katika jamii zao. Data ilikusanywa maktabani, mtandaoni na kuchanganuliwa kwa misingi ya nadharia ya uhalisiajabu iliyoasisiwa na Franz Roh ( 1925). Matokeo ya utafiti wetu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti wetu. Kupitia kwa sifa za wahusika na za mandhari tuligundua kuwa tenzi zimesheheni uhalisiajabu sawia na vipera vingine vya fasihi. Mbali na tenzi zote mbili kudhihirisha sifa za kiuhalisiajabu, ilidhihirika kuwa dhamira za watunzi wa tenzi hizi zimetofautiana mno. Tuligundua kuwa uhalisiajabuhusawiriwa vyema katika mandhari, wahusika wenye sifa za kibinadamu na wale wasiokuwa na sifa za kibinadamu. Aidha tulibaini kuwa wahusika wa aina hizi zote, ni sehemu muhimu katika kujenga historia yajamii zao na dunia yote kwa ujumla.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUhalisiajabu unavyojitokeza katlka ukawafi wa Miiraji na utenzi wa Fumo Liyongoen_US
dc.titleUhalisiajabu unavyojitokeza katlka ukawafi wa Miiraji na utenzi wa Fumo Liyongoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States