Show simple item record

dc.contributor.authorMenya, Ochieng V
dc.date.accessioned2021-10-18T07:58:06Z
dc.date.available2021-10-18T07:58:06Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155608
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza jinsi sitiari za Kiswahili hujitokeza katika kauli za wanasiasa na jinsi wanasiasa huweza kuzitumia kueneza kauli za kichochezi nchini Kenya. Vile vile, jinsi lugha ya Kiswahili ijapokuwa ni lugha rasmi na ya kitaifa inayotakikana kuunganisha wananchi huchangia kueneza kauli za kichochezi katika siasa nchini Kenya, jinsi lugha ya Kiswahili huweza kutumiwa kama chombo cha kuleta uwiano wa kijamii nchini Kenya. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchambua matumizi ya sitiari za Kiswahili katika kauli ya kichochezi kwenye diskosi ya kisiasa nchini ili kubaini na kuchunguza michango yao katika kueneza kauli za kichochezi katika siasa za Kenya. Utafiti huu ulinuia kuchangia pakubwa katika tafiti zilizopo, na kuongeza maarifa mapya katika pengo la kiusomi katika eneo la mchango wa sitiari za Kiswahili katika kauli za kichochezi kwenye diskosi ya kisiasa nchini Kenya. Njia ya utafiti ya mtandao wa Youtube, maktabani na data kutoka kwa tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) ilitumika kuleta maelezo ya mada chini ya uchunguzi kwa kutumia nadharia ya vitendo usemi. Data ilichambuliwa kwa kuzihusisha na malengo ya utafiti. Utafiti huu umebaini kuwa, sitiari ina mchango mkubwa katika semi zozote, inachangia pakubwa katika kueneza kauli ya chuki katika siasa nchini Kenya kwa kuwagawanya na kuwadunisha jamii lengwa. Wanasiasa mara nyingi hutumia sitiari kwenye matamshi yao kwenye kampeni kwa njia ya kushawishi wafuasi wao na pia kuwachochea dhidi ya jamii pinzani. Lugha ya Kiswahili ijapokuwa ni lugha ya taifa na rasmi nchini Kenya ina mchango katika kueneza kauli ya chuki siasani kwa kutumia msamiati ambao wanasiasa hutumia kama matusi dhidi ya jamii nyingine. Vile vile, lugha ya Kiswahili inaweza kutumika kuleta uwiano wa kijamii nchini Kenya. Hata hivyo, licha ya kubuniwa kwa sheria na sera za kukabili hotuba na matamshi ya chuki nchini Kenya, bado kuna changamoto zinazozuia makabiliano dhidi ya kauli ya chuki katika siasa.en_US
dc.language.isoOTHERSen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMchango Wa Sitiari Za Kiswahili Katika Kauli Za Kichochezi Kwenye Diskosi Ya Kisiasa Nchini Kenyaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States