dc.description.abstract | Tasnifu hii inashughulikia fani katika riwaya tatu za Katama
Mkangi. Kazi hizi ni: Ukiwa (1975), Mafuta (1984) na Walenisi
(1995) .
Katika tasnifu hii kuna sura tano. Sura ya kwanza ni pendekezo
la utafiti ambapo turnejadili sorno letu la utafiti, madhurnuni,
sababu za kulichagua sorno hili, mipaka na upeo wa tasnifu,
haipothesia, yaliyoandikwa kuhusu sorno letu, msingi wa
nadharia na njia za utafiti wetu.
Sura ya pili ni uainishaji wa kiutanzu wa kazi za Katama
Mkangi.
Katika sura hii turnejadili dhana za hadithi fupi, novela na
riwaya na kisha kutoa tathmini ya kazi za Mkangi na
kuziainisha kila moja katika utanzu wake rnwafaka.
Katika sura ya tatu turnejadili vipengele vya kirnuundo katika
kazi za Mkangi.Turnerejelea ploti na uumbaji wa wahusika katika
kazi hizi.
Sura ya nne inachunguza mbinu za kirntindo zinazojidhihirisha
katika kazi za Mkangi na sura ya t ano ni hitirnisho la
tasnifu.Baada ya sura ya tano kuna marejeleo ya tasinifu nzima.
Tanbihi zinapatikana
chini ya ukurasa ambapo zinatokea. | en_US |