Show simple item record

dc.contributor.authorKatui, Simon P
dc.date.accessioned2022-04-25T12:41:25Z
dc.date.available2022-04-25T12:41:25Z
dc.date.issued2020
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/160229
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uchanganuzi wa maana ya kipragmatiki katika mawasiliano ya jukwaa la Facebook. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza suala la maana ya kipramatiki katika mawasiliano ya jukwaa la Facebook na malengo maalum yakiwa ni; kubainisha maana ya kipragmatiki katika mawasiliano ya Facebook, kujadili mikakati ya usimbwaji na upanuzi wa maana na kujadili mikakati ya ubanaji wa lugha inavyotumika katika mawasiliano ya jukwaa la Facebook. Data iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu ilitolewa kutoka intaneti kwa makundi ya wanafunzi wa chuo kikuu ambao huwasiliana kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika jukwaa la Facebook. Makundi ambayo yaliteuliwa kutumika katika utafiti huu ni; Kenyan university students, K.U. comrades forum na Kenya university organization. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya pragmatiki leksika ya Blutner (1990), ambapo matokeo ya utafiti huu yamebainika kuwa , wanafunzi wa chuo kikuu huwasiliana kwenye jukwaa la Facebook kwa matumizi ya michakato ya kipragmatiki ambayo ni; upanuzi wa maana, ubanaji wa maana na kisio la maana. Isitoshe, imebainika kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wa chuo kikuu huwasiliana katika jukwaa la Facebook kwa kutumia mchakato wa upanuzi wa kimaana, ikifuatwa na mchakato wa ubanaji wa maana huku asilimia ndogo zaidi ya wanafunzi wa chuo kikuu ikiwasiliana kwa matumizi ya mchakato wa kipragmatiki wa kisio la maana.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUchanganuzi Wa Kipragmatiki Wa Maana Ya Mawasiliano Katika Jukwaa La Facebooken_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States