Show simple item record

dc.contributor.authorKirui, Simon K
dc.date.accessioned2022-04-28T04:04:16Z
dc.date.available2022-04-28T04:04:16Z
dc.date.issued2021
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/160318
dc.description.abstractTasnifu hii ililenga kubainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu: kubainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo, kubainisha jinsi urejelezi ulivyotumika kuleta mshikamano katika gazeti la Taifa Leo na kubainisha iwapo nadharia ya Sarufi Amilifu na nadharia ya Uhusiano zinaweza kutumika kuonyesha umuhimu wa urejelezi katika kuleta mshikamano katika gazeti la Taifa Leo. Data iliyotumika kufikia malengo haya ya utafiti ilitolewa kutoka Habari za Kaunti katika gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya Sarufi Amilifu iliyoendelezwa na Halliday (1985, 1994, 1999), Halliday na Matthiessen (2004) na Matthiessen (2013) ilitumika katika utafiti huu kwa kuangazia mtazamo wa Halliday (1976). Aidha, nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Wilson (2003) na Wilson na Sperber (2002) ilitumika kama nadharia changizi katika kufafanua jinsi wasomaji wanavyofikia maana tambuzi katika matini. Data ya utafiti huu imechanganuliwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa urejelezi wa kiendofora, urejelezi nafsi, urejelezi wa kuashiria na urejelezi wa kulinganisha umetumika katika Habari za Kaunti ili kuleta mshikamano katika matini. Data ya utafiti huu imewasilishwa kwa kutumia maelezo na majedwali kuonyesha jinsi aina mbalimbali za urejelezi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUrejelezi Katika Gazeti La Taifa Leo: Mtazamo Wa Kipragmatikien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States